ETI WEMA AMFUNGIA DIAMOND MPK KASHKNDWA KUHUDHURIA MAZISHI YA GURUMO!

HAYA yanaweza kuwa ni mambo ya malovee !
Kuna madai kwamba Mbongo Fleva Nasibu
Abdul ‘ Diamond ’ alishindwa kushiriki zoezi la
kuuaga mwili wa mwanamuziki mkongwe
Tanzania , marehemu Muhidin Mwalimu
Mohamed Gurumo ‘ Maalim Gurumo’ kwa
sababu alifungiwa asitoke ndani na
mwandani wake madam Wema Sepetu ,
Ijumaa linakudadavulia .
Wema Sepetu na Diamond wakiwa faragha .
Imedaiwa kuwa , Wema alimfanyia ‘ umafia ’
mpenzi wake huyo, Aprili 15, mwaka huu
ambapo ilikuwa ndiyo siku ya mwili wa
marehemu huyo kuagwa nyumbani kwake
Mabibo jijini Dar na kwenda kuzikwa kijijini
Masaki, Kisarawe, Pwani.
Itakumbukwa kuwa , Diamond ndiye msanii
aliyewahi kumpa zawadi ya gari marehemu
Gurumo kutokana na kuguswa na mchango
wake katika tasnia ya muziki nchini .
Diamond akimsaidia mzee Gurumo kupanda
stejini kabla ya kumkabidhi gari Agosti 29 ,
2013 .
Kwa mujibu wa mashuhuda, kitendo cha
Diamond kutoonekana katika mazishi hayo ni
kama amejishushia heshima kubwa
aliyojijengea pale alipomthamini marehemu
huyo kwa kumpa gari aina ya Toyota
FunCargo.
“Tulitegemea tungemuona msibani lakini kwa
kutokuwepo kwake ni kama mchango wake
wa kumpa gari Gurumo hauna maana ,”
alisema shuhuda mmoja aliyekuwepo msibani
hapo.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi
nyumbani kwa marehemu Gurumo na
kujumuika na waombolezaji .
Mwili wa mwanamuziki mkongwe Tanzania ,
marehemu Muhidin Mwalimu Mohamed
Gurumo ukiingizwa kaburini .
Baada ya mapaparazi wetu kufanya upekuzi
yakinifu msibani hapo , walibaini kuwa ,
Diamond hakutia ‘ maguu ’ hivyo shughuli ya
kumsaka ikaanza .
Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu
ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza - Mori
jijini Dar ambako hawakumkuta .
Mapaparazi hawakuchoka , wakahamishia
‘ majeshi ’ nyumbani kwa mwanandani wake
Wema , Makumbusho, Dar ambako mlinzi
alibainisha kuwa , Diamond yupo na ‘ bebi ’
wake Wema .
Mzee Maalim Gurumo enzi za uhai wake.
Mapaparazi waliondoka na kurudi tena saa
8: 37 mchana ambapo pia waliambiwa
wapendanao hao bado wamejifungia ndani,
wakaondoka hadi muda wa jioni baada ya
shughuli za mazishi , walirejea na kuambiwa
Diamond alitoka muda si mrefu pasipo
kujulikana alikoelekea .
Waandishi wetu walimvutia waya Diamond
lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila
kupokelewa.
Kusaka data zaidi , mapaparazi wetu
walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu
Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond
alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda
Kisarawe ambako mazishi yalifanyika .
Mzee Gurumo akionyesha ufunguo wa gari
alilozawadiwa na Diamond.
“Tulikuwepo nyumbani kwa marehemu.
Nilikuwa mimi na Diamond tena tumefika
muda huohuo ndiyo mwili ukawa unapelekwa
kwenye gari . Huwezi amini tulijumuika
kuupandisha mwili kwenye gari na sisi
tukarudi nyumbani kuendelea na shughuli
zetu, ” alisema Babu Tale.
Mapaparazi wetu baada ya kutoshibishwa na
maelezo hayo, juzi Jumatano walimtwangia
simu Diamond ambaye alizungumza kwa
‘ kujikanyagakanyaga ’ .
Diamond na mpenzi wake Wema katika pozi.
“Mh! Nilikuwepo msibani ila sikwenda kuzika
tu maana nilikuwa na Babu Tale pale na
tulikuwa karibu kabisa na gari la Global
Publishers, mara tu baada ya kumaliza
kuupandisha mwili wa marehemu kwenye
gari tuliondoka na kurejea kwenye majukumu
yetu, ” alisema Diamond .
Mapaparazi wa Global walikuwa jirani na gari
alilotaja Diamond lakini hawakumuona staa
huyo achilia mbali waombolezaji wengine
ambao waliuliza kwa nini msanii huyo
hakufika kwenye msiba wa rafiki yake
mkubwa!

0 comments:

Post a Comment