KAJA ALA SHAVU!

Staa maarufu wa filamu hapa Bongo, Kajala
Masanja hivi karibuni alipata shavu la nguvu
baada ya kuibuka kuwa balozi wa wanawake
Tanzania nzima kupitia taasisi ya Women
Connect iliyopo jijini Dar .
Staa maarufu wa filamu hapa Bongo, Kajala
Masanja .
Akizungumza na Ijumaa , mkurugenzi wa
taasisi hiyo , Hafsa Semdaiya alisema
wameamua kumchagua Kajala kwa kuamini
ni kioo cha jamii na ni staa wa kwanza
kuonesha moyo wa kuitikia wito kwani
alianza kwa kutoa misaada kwenye kituo cha
watu walioathirika na madawa ya kulevya.
“Kwa kweli kigezo kikubwa tulichokiona kwa
Kajala ni moyo wake wa kujitoa na pia
tumemuona ni kioo cha jamii na kama
mwanamke anayejali , amekuwa mstari wa
mbele kwenye kutoa misaada mbalimbali
kwa watu wenye uhitaji , ” alisema Semdaiya .
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa , taasisi hiyo
inajihusisha na vitu vingi ila Kajala atahusika
zaidi na kuchangisha fedha ndani na nje ya
nchi kwa ajili ya kuwasaidia wanawake
wenye vimbe mbalimbali .

0 comments:

Post a Comment