MAJIRANI WAMLALAMIKIA JAYDEE

MAJIRANI wanaoishi karibu na mwanamuziki
wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura
‘ Jide ’ wamelalamika kwamba mwanamuziki
huyo ameiweka nyumba yake katika
mazingira ya uchafu yanayohatarisha maisha
yao.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo , Judith
Wambura ‘ Jide’.
Wakizungumza na Amani, majirani hao
wanaoishi Kimara - Temboni jijini Dar ,
walisema mwanadada huyo ameacha vichaka
vikubwa vinavyoizunguka nyumba yake hali
ambayo ni hatari kwani nyoka wanaweza
kufanya makazi hivyo kusababisha maafa
kwa watoto na watu wazima .
“Yaani huyu mwanamuziki Jaydee
ametuachia kichaka , yeye na mumewe
hawataki kufanya usafi kuizunguka nyumba
yao hali ambayo inatupa wasiwasi sisi
majirani, tuna watoto wanaweza kung’ atwa
na nyoka kwani nyoka hupenda kuzaliana
kwenye vichaka kama hivi , ”
alisema jirani mmoja ambaye hakutaka
kutajwa jina lake gazetini.
Waliendelea kusema kuwa , Jide hana
hausigeli wala ndugu yeyote anayeishi naye ,
inawezekana ndiyo maana anashindwa
kufanya usafi kuzunguka nyumba yake.
“Lady Jaydee anaishi na mumewe ( Gardner )
tu labda ndiyo sababu ya kushindwa kutunza
mazingira, majani yameota mpaka kero.
Tumeshapeleka malalamiko yetu serikali ya
mtaa lakini hajaitwa kuambiwa,
tunashangaa, ” alisema jirani huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo , gazeti hili
lilimtafuta Jide na mumewe Gardner ambapo
mume huyo ndiye aliyepatikana na kusomewa
madai hayo. Baada ya kusikiliza mpaka
mwisho , Gardner alijibu :
“Kama wamesema hivyo mimi sina la kujibu
( no comment )” .
Juzi , mapaparazi walifika kwenye ofisi ya
serikali ya mtaa lakini ilikuwa imefungwa.

0 comments:

Post a Comment