JOHARI:HARUSI YA RAY NA CHUCHU NTAKUWA KAMATI YA CHAKULA

MKONGWE kwenye sanaa Bongo, Blandina
Chagula ‘ Johari’ amefunguka kuwa endapo
ikitokea mkurugenzi mwenzake, Vincent Kigos
akaoa, yeye atajitolea kuwa mwandaaji wa
chakula .
Mkongwe kwenye sanaa Bongo , Blandina
Chagula ‘ Johari’ .
Akizungumza na mwanahabari wetu
mwishoni mwa wiki iliyopita, Johari alisema
yeye na Ray ni watu wa karibu kwa kuwa
wameiongoza kampuni yao kwa muda mrefu
hivyo katika jambo muhimu kama la ndoa ,
lazima ajitoe kinaga ubaga kufanikisha .
Msanii wa Bongo Muvi , Vincent Kigosi ' Ray ' .
“Yani hata kama ikitokea kesho mkasikia Ray
anaoa ujue kabisa nitakuwa muandazi
kuhakikisha madikodiko yanawafikia
waalikwa kwa wakati muafaka , ” alisema
Johari ambaye mara zote amekuwa
akikanusha kuwa uhusiano wa kimapenzi na
Ray .

0 comments:

Post a Comment