Kha ! Katika hali isiyoitarajiwa , nyota wa
sinema za Kibongo, Elizabeth Michael
Kimemeta ‘ Lulu’ amejikuta akiangua kilio cha
ukweli kama mtoto kufuatia kuogeshwa kwa
pombe mwilini , jambo ambalo hakulitarajia,
Risasi Jumamosi limetonywa .
Nyota wa sinema za Kibongo , Elizabeth
Michael Kimemeta ‘Lulu ’ akimwagiwa pombe
kwenye birthday yake .
Tukio hilo la aina yake lilijiri Aprili 16, mwaka
huu ndani ya Hoteli ya Regency , Mikocheni
jijini Dar es Salaam ambapo
Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya lulu
marafiki wa Lulu wasio mastaa
walimwangushia ‘ sapraizi’ ya nguvu ya
kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa
( bethidei) . Kwa mujibu wa chanzo makini
ambacho kilizama ndani ya sherehe hiyo bila
waalikwa wote kujua kuwa ni ‘ shushushu’ wa
kujitegemea, Lulu aliitwa kwenye sherehe
hiyo akiwa hajui kitu japokuwa akilini mwake
alitambua kuwa siku hiyo ni bethidei
yake.
TAARIFA YA AWALI
Awali, Risasi Jumamosi lilitonywa na
mtonyaji wake wa habari za mastaa wa
Bongo kwamba, Lulu siku hiyo anafanya
bethidei ya
nguvu maeneo ya Mikocheni lakini eneo
sahihi likiwa halijulikani .
“Jamani nawapa habari ya mjini kama
kawaida yangu . Leo ( Jumatano ) , Lulu
anafanya bethidei . Nasikia ni Mikocheni ,
nimejaribu
kupeleleza ni sehemu gani nimeshindwa , kwa
sababu ninyi ni wadaku hebu jiongezeni
mpeleleze wenyewe ,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza: “Lakini nahisi kuna mazingira ya
usiri. Hakuna staa hata mmoja
atakayekuwepo kwa sababu sherehe yenyewe
imeandaliwa na marafiki zake wa kawaida .”
LULU APIGIWA SIMU , AKIRI, AKWEPA
Baada ya chanzo hicho kuachia taarifa hiyo
nyeti, Risasi Jumamosi lilimsaka Lulu kwa
njia ya simu yake ya mkononi .
Risasi Jumamosi : Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa , niambie .
Risasi Jumamosi : Poa . Tumesikia leo ni
bethidei yako , ni kweli ?
Lulu: Ni kweli ndiyo.
Risasi Jumamosi : Itafanyika wapi ?
Lulu: Mikocheni .
Risasi Jumamosi : Mikocheni sehemu gani?
Lulu: We tambua tu ni Mikocheni , mi
mwenyewe sijui ni sehemu gani ndiyo nataka
kwenda. Kwanza nimefanyiwa sapraizi na
marafiki zangu.
BAADA YA KUPIGWA CHENGA NA LULU
Baada ya Lulu kukwepa kutaja eneo la tukio ,
ndipo timu ya Risasi Jumamosi ikawasiliana
na kamanda wa kikosi maalum cha
Oparesheni Fichua Maovu ‘ OFM ’ na kumpa
kazi ya kujua bethidei ya Lulu itafanyika wapi
katika jijini la Dar es Salaam siku
hiyo .
NDANI YA DAKIKA 45
Ndani ya dakika arobaini na tano, kamanda
wa OFM alirejesha majibu kwamba, sherehe
hiyo itafanyika kwenye Hoteli ya Regency
iliyopo Mikocheni , Dar lakini hakutakuwa na
mastaa na inafanywa kuwa siri ili mapaparazi
wasijue na kufika kupiga picha.
KILICHOTOKEA
Usiku uliingia, Risasi Jumamosi likatia timu
kwenye eneo la hoteli hiyo ambapo
lilibahatika kumpata mtu mmoja akiwa
anaelekea
kwenye sherehe hiyo .
Katika mazungumzo yake na Risasi
Jumamosi , mtu huyo ( jina lipo) alisema kila
kitakachotokea ndani ya shughuli hiyo
atakiweka
wazi ili mradi asitajwe jina gazetini tu !
BAADA YA SHEREHE
Saa saba na nusu usiku , sosi wetu huyo
alilipigia simu Risasi Jumamosi na kuweka
wazi yaliyotokea kwenye bethidei hiyo .
Sosi: Jamani shughuli imekwisha.
Risasi Jumamosi : Nini kimetokea?
Sosi: Lulu aliogeshwa pombe hivihivi
nikishuhudia. Mbaya zaidi wale
waliomwogesha nahisi walikuwa wanafanya
makusudi, maana
walikuwa wanammiminia kuanzia kichwani
hadi miguuni , yaani mwili wote chapachapa .
Risasi Jumamosi : Mwenyewe alikuwa
anasemaje?
Sosi: Kilio. Lulu Amelia sana. Siyo kwamba
alikuwa analia utani , ukweliukweli. Si unajua
yeye aliacha kunywa pombe tangu ule
mkasa wake na marehemu Steven Kanumba ,
sasa leo kuogeshwa pombe hiyohiyo mwili
mzima, nadhani ndiyo maana amelia sana.
MAMA YAKE AMSHANGAA
“Ilibidi Lulu ampigie simu mama yake
( Lucresia Karugila ) na kumweleza
yaliyomkuta, akajuta hata kuhudhuria. Mama
alishangaa
lakini alimuuliza kama yupo salama akasema
yupo salama , ” alisema shushushu wetu.
LULU ABADILI NGUO
Sosi huyo aliendelea kuweka wazi kwamba,
baada ya kuwa chapachapa kwa kulowa
pombe, Lulu aliyetengenezewa keki tano,
alilazimika kwenda kuoga na kubadili nguo
mara mbili . Mwisho alivaa gauni la rangi ya
kahawia .
“Naamini alibadili hata nguo za ndani , maana
alilowa pombe mwili mzima, ” kilisema chanzo
hicho huku kikisisitiza kwamba jina
lake liwekwe kapuni.
MASTAA WAKAUKA
Ilidaiwa kuwa tofauti na shughuli nyingine za
mastaa ambapo mastaa wenzake hujaa ,
bethidei hiyo ya Lulu mtu mwenye jina kubwa
Bongo aliyehudhuria sherehe hiyo ni Mahsin
Awadh ‘ Dk . Cheni ’ peke yake .
KWA MAANA HIYO
Kwa sherehe hiyo , Lulu ametimiza miaka 19
tangu kuzaliwa kwake. Alizaliwa Jumapili ya
Aprili 16 , 1995 .
LULU AOGESHWA POMBE KWENYE BIRTHDAY YAKE
1:57 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment