KUNANI HAPA??

Pamoja na kuenea kwa picha zenye utata, rapper
wa Kenya, Nazizi aliwahi kukanusha taarifa kuwa
ana uhusiano wa kimapenzi na producer kutoka
Mwanza, Tanzania, Sappy ambaye kwa sasa ni
mtayarishaji wa Homeboyz Production ya Kenya,
wawili hao wameendelea kuwa karibu kiasi cha
kutoonesha ‘uhusiano wa msanii na producer’
wake kama walivyosema.
Penzi la Sappy na Nazizi limeendelea kushamiri
kiasi cha producer huyo kuamua kumpeleka kwao
Mwanza kumtambulisha kwa wazazi wake.
Isitoshe, Sappy amekuwa karibu mno na familia
ya Nazizi kiasi ambacho hadi mtoto wa Nazizi
amemzoea Sappy ‘anayeplay role’ ya ubaba kwa
sasa baada ya Nazizi kuachana na mume wake.

Wawili hao pia wamerekodi wimbo wa pamoja
uitwao Gangster Love.

0 comments:

Post a Comment