KAJALA AONYESHA JEURI YA PESA KWA WANA BONGO MOVIES..!! SOMA HAPA


MSANII wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja
hivi karibuni alionesha jeuri ya magari baada ya
kutinga nayo mawili kwa nyakati tofauti kwenye
kumbukumbu ya miaka miwili ya marehemu
Steven Kanumba.
Muonekano wa ndani wa gari aina ya Toyota
Bravis anayomiliki Kajala.
Awali kwenye ibada ya kumuombea marehemu,
Kajala alifika kwenye kanisa moja lililopo
Kimara Temboni akiwa ‘anadraivu’ gari aina ya
Toyota Harrier nyeusi na kuzua gumzo eneo hilo
Kajala Masanja.
Baadaye msafara ulipohamia Makaburi ya
Kinondoni alipozikwa Kanumba, alitinga na gari
lingine aina ya Toyota Brevis lile ambalo ilidaiwa
kuwa alinunuliwa na yule kigogo wa shosti
wake, Wema Sepetu anayejulikana kwa jina la
CK. Jeuri hiyo iliwafanya wengi kubaki na vingi
viulizo na Ijumaa lilipojaribu kumdadisi hakutoa
ushirikiano na hata alipopigiwa simu baadaye
hakupatikana hewani

0 comments:

Post a Comment