AKAMATWA KWA KULA MAITI YA MTOTO!

Ni visa mbavyo wengi tulivisikia katika
hadithi za kale , watu kuliwa na majitu, lakini
katika siku za karibuni tumeshuhudia watu
wakila viungo vya wenzao Jamhuri ya Afrika
ya Kati katika jazba ya kulipiza kisasi dhidi
ya watu waliowadhulumu katika uongozi
uliong' olewa mamlakani wa Seleka .
Nchini Pakistan Polisi wamewakamata
wanaume wawili kwa makosa ya kuiba maiti
ya mtoto kutoka kaburini na kisha kumla.
Wawili hao Arif Ali na kakake Mohammed
Farman Ali waliachiwa huru baada ya kuwa
jela kwa miaka miwili kwa kula nyama ya
binadamu.
Hata hivyo wawili hao wameonekana kuwa
na tamaa kubwa ya mchuzi wa nyama ya
binadamu.Wakaazi hao wa kijiji cha Daryabn
Khan jimbo la Punjab walikamatwa mwaka
2011.
Polisi walisema kwamba walipata kiwiliwili
cha maiti ya msichana mdogo kikiwa bila
miguu na mikono. Wawili hao walikiri kwamba
walipika mchuzi wa nyama ya viungo hivyo
na kuvila .
Walishtakiwa kwa makosa ya kuharibu kaburi
kwani nchini Pakistan hakuna sheria
inayozungumzia hatia ya mtu kumla
mwenzie.
Punde baada ya kuachiwa Arif Ali aliambia
BBC kwamba anajutia makosa hayo na
kwamba hatarudia tena .
Hata hivyo punde si punde polisi wamesema
waliitwa na majirani wa jamaa huyo
wakilalamikia uvundo mkali kutoka kwa
nyumba yake .
Walipoingia chumbani humo Lo ! wakapata
kichwa cha mtoto . Kiwiliwili hakijulikani
kililiwa au kapotelea wapi . Arif Ali tena
amekamatwa kwa mara ya pili na polisi
wanaendelea kumsaka kakake .
Polisi wanaamini ndugu hawa walifukua maiti
ya mtoto ambaye kichwa kilipatikana ndani
ya makaazi yao.Arif anamlaumu kakake
Farman. Wawili hao waliwahi kuoa na hata
wakajaliwa watoto , hata hivyo wake zao
waliwatoroka kabla ya kukamatwa kwao na
kufungwa jela kwa kisa cha awali .
CHANZO NI BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment