HAMMER Q AJIONDOA KWENYE KUNDI LA OFFSIDE TRICK


Msanii wa muziki wa Taarab na Bongo
Flava, Hammer Q amejiondoa kwenye kundi
la muziki la Offside Trick baada ya kuona
hanufaiki na chochote.
Hammer Q ameiambia BK kuwa kwa sasa
atakuwa akifanya kazi zake mwenyewe.
“Kwasasa hivi nimeamua kujishughulisha
na mishemishe zangu mwenyewe
kwasababu nimejiunga Offside Trick muda
kidogo kama miaka miwili,lakini
kilichotokea pale ni uvivu katika issue za
kazi, yaAni kwamba mkisharekodi watu
wanakuwa wavivu kufuatilia mambo ya
kazi,sasa ile kwa upande wangu naona
kama inanirudisha nyuma,” alisema.
“Sasa nikaona kwasababu mimi nina uwezo
wangu binafsi tukiacha masuala ya Offside
Trick niamue kwanza kufanya kazi kwanza
mwenyewe,hakuna ugomvi uliotokea
kwasasabu mimi mwenyewe binafsi yangu
mambo ya ugomvi huwaga siyapendi, lakini
kilichotokea kwangu mimi ni maslahi ya
kuendelea kukaa pale,kwasababu tunaweza
tukapanga tufanye dili hili na hili
tukajiandalia show halafu mwisho wa siku
mshikaji akachomoa, sasa hizi ni lawama
na tunaharibiana kwa wale waandaji wa
show wenyewe. Ukiangalia vitu kama hivyo
ni moja wapo vimenisababisha nianze
kufanya kazi zangu. Tunaweza tukapata
issu sehemu fulani tukaalikwa, mshikaji
anakataa kwasababu yeye ana studio
inaingiza, mimi sina studio nategemea
muziki ndio kazi yangu,” alisema Hammer
Q.
Hammer Q amesema yeye na AT aliyejitoa
kwenye kundi hili muda mrefu uliopita
wamerekodi wimbo uitwao ‘Siri’.
“Kuna kazi nafanya mimi na AT nadhani
next wiki itakuwa ipo tayari,” amesema
msanii huyo. “Mimi ni mkubwa sana katika
muziki ugomvi wowote ambao umetokea
mimi siuangalii kwababu sisi wote
tumetoka kumoja,hatuitaji kushadadia issue
za ugomvi kama hizo. Sijataka kuangalia
chanzo cha ugomvi mimi nimeangalia
uwezo wa kazi, kwamba nikikaa mimi na
AT tunaweza tukafanya kitu kimoja kizuri
sana. Kwahiyo sijataka kuangalia issue za
ugomvi nataka tuonyeshe uwezo wa kazi,
mimi na AT kila mmoja anafanya kazi
kivyake sema sasa hivi kuna kazi ambayo
nimeamua nifanye na AT kwa kipindi
hiki,hatuzungumzii kundi, kila mmoja
anatambua uwezo wa mwenzake ndio
maana akakubali kufanya kazi na mimi.
Hata mimi naelewa yeye ana uwezo wake
binafsi ndio maana mimi nikakubali kufanya
kazi na yeye,kwahiyo tunafanya kazi kama
watu wawili yaani mimi na yeye, lakini sio
kundi.”

0 comments:

Post a Comment