CHUCHU PIGA , UA LAZIMA RAY ATANIOA !


LICHA ya hivi karibuni gazeti dada la hili ,
Risasi kumnukuu mcheza filamu mahiri
Vincent Kigosi ‘ Ray ’ akikana kuwepo kwa
mpango wa kumuoa mpenzi wake Chuchu
Hans, dada huyo ambaye pia ni msanii wa
fani hiyo , ameibuka na kusema piga ua
lazima wataoana.
Vincent Kigosi ‘Ray ’ akiwa kwenye pozi la
kimahaba na Chuchu hans
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Chuchu
alisema hana uhakika kama mpenzi wake
huyo alimaanisha kile kilichoandikwa gazetini
kwa vile ana mapenzi ya dhati kwake.
Vincent Kigosi ‘ Ray ’
“Kiukweli mimi moyo wangu unakataa kama
alisema maneno hayo kwa vile ni mtu
ambaye namjua ana mapenzi ya dhati
kwangu , ” alisema .
Chuchu Hans
Mwanadada huyo aliongeza kuwa , anahisi
kuna kidudu mtu mwenye nia ya kuleta
mtafaruku ndani ya uhusiano wao kwa
kuchochea fitina ili mapenzi yao yavurugike.
“Unajua kuwa kuna uwezekano kabisa kuna
kidudu mtu ambaye anataka kuleta mtafaruku
ili tugombane bila sababu na hilo mimi
sikubaliani nalo, ” alisema .

0 comments:

Post a Comment