ACHOMWA KISU KISA MUME WA MTU !


JESHIla polisi mkoani hapa linamshikilia
mwanamke aliyejulikana kwa jina la Pima
Mabubu kwa tuhuma za kumchoma kisu
mpaka kumjeruhi vibaya mwanamke
mwenzake, Amina Hussein akidai ana
uhusiano wa kimapenzi na mumewe, Adam
Ndekeja , Risasi Jumamosi lina mkasa wote .
Amina Hussein akipata matibabu katika
hospital ya taifa Muhimbili.
Tukio hilo lililowaacha watu vinywa wazi ,
lilijiri Aprili 22, mwaka huu shambani katika
Kijiji cha Kigwa, Kata ya Ukondamoyo
wilayani Uyui , Mkoa wa Tabora .
KISU KILIVYOFANYA KAZI
Habari kutoka kwa baadhi ya mashuhuda
zinasema kuwa , Amina alichomwa kisu mara
mbili, kwenye paja mguu wa kushoto kisha
kwenye mgongo ambapo kilizama na kutoka
mpini tu !
Amina Hussein akikimbizwa hospital baada
ya kupatwa na mkasa huo.
KISA KINASIMULIWA
Kwa mujibu wa taarifa za awali , siku ya
tukio, Pima alitoka nyumbani kwake na
kumfuatilia mumewe huyo kwenye shamba la
tumbaku la kaka wa Amina ( jina
halikupatikana ) ambako alisikia kuwa
mwanamke huyo yupo na mumewe.
“Pima alisikia Amina ana uhusiano na
mumewe. Siku hiyo akasikia wapo shambani .
Akatoka nyumbani na kufuatilia akijua
atawanasa laivu , ” kilisema chanzo hicho.
Kisu kinachosadikika kilitumika kumjeruhi
Amina Hussein.
MWANAMKE ALIYECHOMWA KISU
Akizungumza akiwa amelazwa akiuguza
majeraha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Tabora , Kitete , Amina alisema :
“Mimi sina uhusiano na huyo mwanaume
jamani. Kwanza huyo mwanamke simjui
kabisa . Nimemwona kwa mara ya kwanza
siku hiyo ya tukio .
“Siku hiyo mimi na mwanangu kichanga ( wa
miezi mitatu ) tulikuwa shambani , mimi
nilikuwa nikimsaidia kaka yangu kuvuna
tumbaku, akaja Adam ( mwenye mke ) naye
akawa anasaidia kuvuna. Kuna wakati
nilikwenda kupumzika mahali ili
nimnyonyeshe mwanangu .
“Ghafla aliibuka huyo mwanamke. Nilimwona
akinifuata mimi moja kwa moja. Aliponifikia
alinirukia na kuanza kunichoma kisu
mgongoni na kwenye paja la kushoto .
“Ilikuwa ni hatua chache tu tokea mahali
ambako mume wake alikuwa akivuna .
Nilipiga kelele za kuomba msaada , mume
wake akaja mbio kusaidia kwa kumdhibiti
mke wake asiendelee kunichoma kisu zaidi , ”
alisema Amina.
Akaendelea : “Nilianguka chini na kuanza
kugalagala huku damu nyingi zikinitoka .
Ndipo wasamaria wema nao walifika na
kumkamata Pima , wakamfunga kamba na
kumpeleka ofisi ya kata ambako alipelekwa
Kituo Kikuu cha Polisi Tabora . ”
BODABODA YAMKIMBIZA HOSPITALI
Habari zaidi zinasema kuwa , Amina akiwa hoi
na damu chapachapa , alipandishwa kwenye
bodaboda na kukimbizwa kweynye hospitali
ya rufaa ya mkoa kwa ajili ya matibabu huku
hali yake ikionekana si ya kuridhisha.
KILA MTU NA WAKE
Taarifa zaidi zinasema kuwa , wakati ndugu
wa Amina wakihaha kumshughulikia majeruhi
huyo kupata matibabu kwa lengo la kuokoa
uhai wake , baadhi ya ndugu wa Pima
walipiga kambi nje ya kituo cha polisi
wakipigania kumdhamini ndugu yao huyo.
“Ukitaka kujua msemo kwamba kila mchuma
janga hula na wa kwao fuatilia mkasa huu.
Wakati ndugu wa Amina wakihaha kuokoa
maisha yake hospitalini, ndugu wa Pima nao
walikuwa wakihangaika kuhakikisha
mtuhumiwa huyo anapata dhamana ili arejee
uraiani . Hakuna aliyekwenda kumjulia hali
Amina,” kilisema chanzo.
KUHUSU MUME WA MTUHUMIWA
Katika hali isiyotarajiwa , mume wa
mtuhumiwa huyo alikimbia kusikojulikana
muda mfupi baada ya mkasa huo kutokea
jambo ambalo limezua maswali yasiyo na
majibu.
Wengi wamekuwa wakiuliza ni nini
kimemkimbiza mwanaume huyo kama kweli
yeye hana uhusiano wowote na mwanamke
huyo?!
“Au kuna ukweli unafichwa? Kama hakuna ni
kwa nini Adam alikimbia? Hapa kuna haja ya
jeshi la polisi kumsaka mwanaume huyo
mpaka kumkamata ili ukweli ujulikane ,”
alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.

0 comments:

Post a Comment