Mwili wa marehemu Anastazia
Lackfordukiagwa kabla ya kwenda kuzikwa .
Mwili wa marehemu Anastazia Lackford
ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya
Sekondari Mwanza, umezikwa juzi katika
makaburi ya Lunala , Manispaa ya Ilemela
mkoani Mwanza lakini simulizi ya baba
mzazi wa marehemu, Lackford Magafu
kuhusishwa na kifo cha mwanaye
inashangaza!
Kabla ya kifo.
Mwili wa marehemu Anastazia
Lackfordukiwa kwenye jeneza
Inadaiwa kuwa , Machi 27, mwaka huu baba
wa marehemu , Magafu alimpiga sana mtoto
huyo kwa madai ya kutopika chakula kwa
wakati.
Ilizidi kudaiwa kuwa , mbali na kipigo hicho
mzazi huyo alimmwagia mafuta ya taa na
kumchoma moto , hali iliyomsababishia
majeraha mwilini .
“Baada ya ukatili huo, baba huyo alimchukua
Anastazia na kwenda naye Kituo cha Polisi
cha Igogo ambako alidanganya kuwa ,
mwanaye alilipukiwa na jiko , uongo ambao
marehemu aliukubali ili kumuokoa baba
yake, ” kilidai chanzo kilichoomba hifadhi ya
jina lake .
Ikaelezwa kuwa , mtoto huyo alipelekwa
Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, Butimba ,
baadaye Sekou Toure kabla ya kupelekwa
Bugando na kulazwa wodi ya wagonjwa
mahututi, wanaohitaji uangalizi maalum
( ICU) .
Chanzo cha kifo
Hata hivyo , kifo cha Anastazia kilichotokea
Aprili 16 , mwaka huu hakijathibitishwa
kimesababishwa na majeraha yaliyotokana na
moto au kinachodaiwa kuwa ni sumu
iliyowekwa kwenye juisi inayodaiwa
kupelekwa na Magafu wakati marehemu
alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya
Bugando.
Mmoja wa watu waliokuwa wakimuuguza
Anastazia ( jina linahifadhiwa ) alidai kuwa ,
siku hiyo Magafu alipeleka juisi hiyo na
baada ya mgonjwa kuinywa alianza kujisikia
vibaya .
Awali, Anastazia aligoma kuinywa juisi hiyo
kana kwamba alihisi kitu lakini baada ya
kulazimishwa aliinywa kwa shingo upande .
“Baba yake alipoondoka tu , Anastazia
akaanza kujihisi vibaya , akawa anatapika
mabonge mabonge ya vitu vyeusi.
“Nilipompigia simu baba yake na kumwambia
hali ya mgonjwa na kumuuliza kama juisi ile
alitengeneza mwenyewe , amenunua au
amepewa , alinijibu kuwa ametengeneza yeye.
“Akaniambia nisimwambie mtu lakini nikaona
ni bora kuwaambie ndugu zake na wauguzi ,
haikuchukua muda mrefu mgonjwa akawa
amefariki , ” alidai mtoa habari huyo bila
kueleza chanzo hasa cha kifo hicho.
Akizungumzia kifo cha mwanaye , mama
mdogo wa marehemu, Nongwa Gilbert
alisema hana cha kusema bali anamwachia
Mungu .
“Nimeshazungumza sana hadi nimechoka,
kilichobaki namwachia Mungu maana hata
nikizungumza sitaweza kumrudisha,” alisema
Nongwa.
Hadi sasa Magafu anashikiliwa na jeshi la
polisi jijini Mwanza na kuhusu juisi aliyopewa
Anastazia kusababisha kifo chake , Kamanda
wa Polisi Kamishna Msaidizi Mwandamizi
( SACP) Valentino Mulowola alisema :
“Uchunguzi ulifanyika , lakini majibu bado
yanasubiriwa kutoka kwa Mkemia Mkuu wa
Serikali ambaye amepelekewa sampuli kwa
uchunguzi wa kisayansi. Suala la mtuhumiwa
kufikishwa mahakamani ni uamuzi wa
Mwendesha Mashtaka wa Serikali ( DPP ) .”
Marehemu alizaliwa Januari 30, 1997 , alisoma
Shule ya Msingi Kirumba kuanzia mwaka
2004, akajiunga Shule ya Sekondari Mwanza
mwaka 2011 . Hadi anafariki dunia alikuwa
kidato cha tatu akichukua masomo ya sanaa.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi-
Amin .
BABA AHUSISHWA KIFO CHA DENTI MWANZA !
11:06 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment