SIKU chache baada ya mwimbaji wa nyimbo
za Injili , Rose Mhando kunusurika kutekwa ,
ujumbe wa tishio la kuuawa kwa Mchungaji
wa Kanisa la Huduma ya Maombezi , Anthony
Lusekelo ‘ Mzee wa Upako’ umesambazwa.
Anthony Lusekelo ‘Mzee wa
Upako ’akisisitiza jambo
Ujumbe huo ambao ulitumwa na mtu
aliyejitambulisha kama msamaria mwema ,
ulisambazwa kwa watu mbalimbali mpaka
kuwafikia mapaparazi wetu, unaeleza
kwamba mbaya wa Rose Mhando ana
mpango wa kumuua Mzee wa Upako.
Uliendelea kufafanua kwamba sababu za
kuuawa kwa mtumishi huyo wa Mungu ni
kwa vile ameonekana kujipendekeza
kumsaidia Rose baada ya tukio lake .
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo, alisema
kwa sasa kanisa lao lipo kwenye maombi
maalumu kwa ajili ya kumuombea kiongozi
wao ili Mungu amuepushe na hila zote za
maadui .
“Hawana uwezo wa kumuua mchungaji wetu
maana amefunikwa na damu ya
Yesu, ”alisema muumini huyo.
Waandishi wetu walifunga safari mpaka
kanisani kwa Mzee wa Upako na kufanikiwa
kuzungumza na msaidizi wa mchungaji huyo
ambaye hakutaka kutajwa gazetini, aliyekiri
kusikia madai hayo, lakini akasema
hawayaamini
UUJUMBE WA KUMTISHIA MAISHA MZEE WA UPAKO
11:04 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment