BABY MADAHA:NITAOLEWA 2030

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby
Madaha amesema hana papara na suala la
ndoa kwani amejipanga kutimiza tendo hilo
mwaka 2030 .
Staa wa muziki na filamu Bongo , Baby
Madaha.
Akizungumza na paparazi wetu, Baby alisema
anachoomba ni uzima kwani suala la ndoa
analiona halina umuhimu kwa sasa kwani ni
kipindi cha yeye kusaka fedha kwa hali na
mali.
“Sina haraka bwana, maisha haya yanahitaji
kuyatengeneza , najipanga Mungu akipenda
labda kwenye 2030 huko ndiyo nitafunga
ndoa sasa hivi acha nitengeneze chapaa ,”
alisema Baby ambaye umri wake unakadiriwa
kutopungua miaka 30 .

0 comments:

Post a Comment