Usiku wa April 13 2014 kwenye
baa iitwayo ‘Arusha night park’
iliyopo Mianzini Arusha ambayo
siku zote ni miongoni mwa
sehemu zinazokua na mkusanyiko
wa watu wengi kuanzia jioni,
limerushwa bomu wakati watu
mbalimbali wakitazama mpira.
Blog hii imepata nafasi ya kuongea na
mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni
kiongozi wa Kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa ambae amethibitisha
kwamba ni watu 15 wamejeruhiwa
kwenye mlipuko huo.
Anasema wote wamepelekwa hospitali
ambapo uchunguzi wa awali
umeonyesha bomu hilo ni la
kutengenezwa kwa mkono na mpaka
sasa hajajulikana alietekeleza
shambulio hilo.
Kwenye sentensi nyingine pia amesema
hakuna aliepoteza maisha kwenye
shambulio hilo ambalo uchunguzi wa
awali umeshatoka, ila baadae itatoka
taarifa rasmi pale uchunguzi kamili
utakapokamilika.
AZUNGUMZIA TUKIO LA BOMU KULIPUKA KWENYE BAA USIKU APRILI 13, 2014
5:35 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment