HARUSI YA MTOTO WA RAISI WA NIGERIA, WAGENI WAALIKWA WAPEWA IPHONE 5 {Gold Plated customized} KILA MMOJA KAMA ZAWADI


Kibongo bongo tumezoea mtu anapotaka
kufunga ndoa lazima ipitishwe michango ya
kutosha ili kuweza kufanikisha sherehe, na pia
mchango wako ndio huwa kiingilio chako yaani
bila kuchanga hupati mwaliko.
Hizi ni zawadi za iPhone 5 walizopewa wageni
waalikwa
Mambo yamekuwa kinyume katika harusi ya
mtoto wa kike wa Rais Goodluck Jonathan wa
Nigeria aitwaye Faith, ambaye katika harusi yake
iliyofanyika jana (April 12) wageni walioalikwa
wamefanyiwa surprise kwa kupewa zawadi ya
simu za iPhone 5 ‘gold plated customized’,
zilizoandikwa majina ya maharusi hao Faith na
Godswill.
Juu ya mabox yaliyokuwa na zawadi ya simu
hizo pameandikwa ‘Leeberry and her Prince wish
you all the best for making our day beautifull.
Thanx for coming and God Bless you’
Cha kusikitisha ni kwamba aina ya wageni
wanaoweza kupata mwaliko wa harusi kama hii
ya mtoto wa mkubwa ni watu wa class flani ya
watu wanaojiweza, hivyo unaweza kukuta ni mtu
ambaye tayari anayemiliki hata iPhones mbili au
tatu, so inakuwa sio big deal kivile! (Nawaza tu
kwa sauti).

0 comments:

Post a Comment