PICHA KUTOKA NYUMBANI KWA MAREHEMU GURUMO USIKU HUU

Maandalizi ya maziko ya Mwanamuziki Mkongwe
Muhidin Gurumo aliefariki saa nane mchana
kwenye hospitali ya taifa Muhimbili bado
yanafanywa ambapo millardayo.com imefika
nyumbani kwa marehemu usiku huu na kuongea
na mtoto wa kwanza wa marehemu Abdallah
Muhidin Gurumo.
Abdallah amesema mpaka sasa kama familia
imeamua maziko yafanyike Jumanne April 15
2014 saa nne asubuhi kwenye kijiji cha Masaki
wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.

0 comments:

Post a Comment