Baada ya mapacha wa P-Square na kaka yao
Jude Okoye kuthibitisha amani imerejea baina
yao, Paul Okoye amezitupia lawama media za
Nigeria kuwa zilikuza ugomvi wao ambao amedai
ulikuwa mdogo na wa kawaida.
“Ugomvi na mgogoro wa mapacha sio kitu
kikubwa ni vile tu Naija media waliukuza kupita
kiasi” alisema Paul.
Paul pia amemtetea mke wa pacha wake Peter
kuwa hakuhusika kwa lolote katika mgogoro wao
hivyo kuwaomba watu wasimlaumu Lola sababu
hana hatia.
Paul aliongeza kuwa watu wasichukulie poa
nguvu ya damu (ndugu) kwa kumaanisha kuwa
sio kitu rahisi kuwatenganisha.
Hiki ndicho alichokiandika Paul Okoye kupitia
ukurasa wake wa facebook jana:
Please whatever happen was not cause by any
woman, pls and pls stop blaming ma brother’s
wife Lola for wat she’s innocent. Twins fight and
quarrel is not a big deal only dat naija media
over-emphasized it, but never underestimate the
power of blood. It’s thicker than water. Much love
to y’all. #Family #ForeverPsquare
Wakati huo huo siku moja baada ya ndugu hao
kuthibitisha kuwa wameyamaliza matatizo yao,
Peter, Paul na Jude Okoye walionekana pamoja
juzi katika sherehe ya model aitwaye Sarah Ofili.
Paul Okoye azilaumu media za Naija kwa kuukuza ugomvi wao, ‘never underestimate the power of blood’
(PIC YA UTUBE NIMEKUPA ILI USERCH VDEO UWEKE NA HII STORY)...... Don’t bring black people to my games’ kauli ya mmiliki wa L.A Clippers, Donald Sterling kwa girlfriend wake yamponza
Mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya Los
Angeles Clippers, Donald Sterling yupo kwenye kiti
moto baada ya maongezi yake na mpenzi wake V.
Stiviano kuvuja ambamo anasikika akitoa maneno
ya kibaguzi dhidi ya Wamarekani weusi.
Mazungumzo hayo yamewekwa kwenye mtandao
wa TMZ ambapo Sterling anamkaripia Stiviano
kwa kuwa karibu na watu weusi na kwa kupost
picha kwenye Instagram akiwa na mchezaji wa
zamani wa Lakers, Magic Johnson.
Maneno aliyosema ni pamoja na: “It bothers me a
lot that you want to broadcast that you’re
associating with black people. Do you have to?
You can sleep with [black people]. You can bring
them in, you can do whatever you want. The little
I ask you is not to promote it on that … and not
to bring them to my games.”
Timu yake inaundwa na wachezaji wengi weusi
wakiwemo Chris Paul na Blake Griffin.
Msemaji wa NBA ametoa maelezo yasemayo: We
are in the process of conducting a full
investigation into the audio recording obtained by
TMZ. The remarks heard on the recording are
disturbing and offensive, but at this time we have
no further information.”
Waziri mkuu wa Korea Kusini ajiuzulu kufuatia kuzama kwa ferry iliyosababisha vifo vya watu 187
Waziri mkuu wa Korea Kusini Chung Hong-won
amejiuzulu kufuatia kuzama kwa Ferry ya Sewol
iliyokuwa na jumla ya abiria 476 wengi wao
wakiwa ni wanafunzi na walimu, huko pwani ya
kusini ya nchi hiyo wiki iliyopita.
“vilio cha familia za wale ambao bado
hawajaonekana vinanikosesha usingizi usiku”
alisema Chung Hong-won.
Maafisa wa Korea Kusini wamethibitisha jumla ya
watu 187 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Wakati akitoa taarifa ya kujiuzulu alisema kitu
sahihi anachotakiwa kufanya sasa ni kuwajibika
na kujiuzulu kutokana na kile kilichotokea, na
kuomba radhi kwa niaba ya Serikali.
Baadhi ya wakazi wa Korea Kusini wakimtazama
Waziri mkuu wakati akijiuzulu
Haya ndio maneno ya Mr Chung aliyoyasema
kupitia televisheni:
“The right thing for me to do is to take
responsibility and resign as a person who is in
charge of the cabinet, on behalf of the
government, I apologise for many problems from
the prevention of the accident to the early
handling of the disaster.”
Aliongeza: “There have been so many varieties of
irregularities that have continued in every corner
of our society and practices that have gone
wrong. I hope these deep-rooted evils get
corrected this time and this kind of accident never
happens again.”
Rais Park Geun-hye wa Korea Kusini
amekubaliana na kujiuzulu wa waziri mkuu wake.
Source BBC
BEHIND ZE SCENE YA WIMBO WA TONTOFLOXY..NASKIA RAHA
Mwanadada Tontofloxy yupo katika kurecord video yake ya wimbo wa nasikia raha chini ya Legendary production inaonekana video itakuwa ni sheeda mtonyaji wetu alibahatika kumfuma location na kumfotoa pic hizi hebu zicheki na wewe.
Story by @GossipCourt
