Waziri mkuu wa Korea Kusini ajiuzulu kufuatia kuzama kwa ferry iliyosababisha vifo vya watu 187


Waziri mkuu wa Korea Kusini Chung Hong-won
amejiuzulu kufuatia kuzama kwa Ferry ya Sewol
iliyokuwa na jumla ya abiria 476 wengi wao
wakiwa ni wanafunzi na walimu, huko pwani ya
kusini ya nchi hiyo wiki iliyopita.
“vilio cha familia za wale ambao bado
hawajaonekana vinanikosesha usingizi usiku”
alisema Chung Hong-won.
Maafisa wa Korea Kusini wamethibitisha jumla ya
watu 187 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Wakati akitoa taarifa ya kujiuzulu alisema kitu
sahihi anachotakiwa kufanya sasa ni kuwajibika
na kujiuzulu kutokana na kile kilichotokea, na
kuomba radhi kwa niaba ya Serikali.
Baadhi ya wakazi wa Korea Kusini wakimtazama
Waziri mkuu wakati akijiuzulu
Haya ndio maneno ya Mr Chung aliyoyasema
kupitia televisheni:
“The right thing for me to do is to take
responsibility and resign as a person who is in
charge of the cabinet, on behalf of the
government, I apologise for many problems from
the prevention of the accident to the early
handling of the disaster.”
Aliongeza: “There have been so many varieties of
irregularities that have continued in every corner
of our society and practices that have gone
wrong. I hope these deep-rooted evils get
corrected this time and this kind of accident never
happens again.”
Rais Park Geun-hye wa Korea Kusini
amekubaliana na kujiuzulu wa waziri mkuu wake.
Source BBC

0 comments:

Post a Comment