HUYU NDIYE ALIYETUNGA JINA LA TANZANIA MFAHAMU KWA UNDANI MOHAMMED IQBAL DAR.


Nimeona niwafahamishe hili huenda likatusaidia
hasa kwa hivi sasa wakati tukisherekea miaka
50 Muungano, najua wengi wetu hatujui historia
ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar  maana tuliwakuta waasisi wetu
wameishafanya zoezi hilo , tusilijadili sana kwa
kuwa lengo lao lilikuwa zuri.
Lakini je unamjua huyu Bwana aliyetunga jina la
Tanzania pata historia ya namnaalivyofanikiwa
kupata jina la TANZANIA.
Sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na
Zanzibar huwa tunasherekea kila Mwaka Tarehe
26/04/ lakini Tangu mimi binafsi nipate
ufahamu na kuanza kushuhudia sherehe za
Muungano nimekuwa nikisikia kuwa jina la
Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika,
Wazanzibar na Raia wengine wa nje lakini
sikuwahi kukutana na huyo ambae alibuni jina
hili tamu la Tanzania .
Imekuwa kama Bahati nimekutana na Mtu huyu
aliyebuni jina la Tanzania Mkoani Mtwara,
sehemu ambayo tayari naiweka kwenye Historia
yangu hata kesho
nikiondokaMtwara nitaikumbuka Radio
yangu Safari Radio.
Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni
Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM
JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED
IQBAL DAR.
Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya
1944, Baba mzazi wa Mohammed alikuwa
Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa
Dr. T A DAR alikuwa Tanganyika kuanzia
mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya
Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D
AGHAKHAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na
baada ya hapo alikuja baadae kujiunga
na Chuo cha Mzumbe akasoma Kidato cha
Kwanza mpaka cha Sita.
Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza jina
la Muungano kati Tanganyika na Zanzibar ?
Mohammed anasema alikuwa Maktaba
akijisoma gazeti la Tanganyika Standard, siku
hizi Daily News, akaona Tangazo linasema
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
unafahamika kama Republic of Tanganyika and
Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo
Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye
shindano la Kupendekeza jina moja litakalo
zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na
Zanzibar Mohammed Iqbal Dar anasema
aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo
alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano.
Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika
Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na
Imani yake na baada ya hapo akaandika jina
la  Tanganyika  baada ya hapo
akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake
Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake
ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena
Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili
apate jina zuri kutoka katika majina hayo
aliyokuwa ameyaandika. Baada ya hapo
Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu
kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande
wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za
Mwanzo ZAN ukiunganisha
unapataTANZAN alivyoona hivyo
akachukua  I herufi ya kwanza katika jina lake
la Iqbal na akachukuaA kutoka jina la dini yake
yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza
herufi hizi mbili I na Akwenye TANZAN unapata
jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona
ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba
akiongeza herufi hizo za I na A kwenye TANZAN
italeta maana kwakuwa nchi nyingi
za Afrika zinaishia
na IA, mfano EthiopIA, ZambIA , NigerIA, TunisIA
, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA,
MauritanIA alivyoona hivyo akaamua
apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike
kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika
na Zanzibar kwa maana hiyo
jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne
majina hayo ni Tanganyika, Zanzibar,
Iqbal na Ahmadiyya.
Mohammed Iqbal Dar baada ya kupata jina hilo
akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu
Shindano. Baada ya Muda mwingi kupita baba
yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua
nzito kutoka Serikalini ikiwa inasomeka kama
ifuatavyo…
                     REPRESENTED BY THE
MINISTRY OF INFORMATION AND
TOURI,TANZANIA TO
MOHAMED IQBAL DAR
IN RECOGNATION OF THE
ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW NAME
FOR THE
UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND
ZANZIBAR NAMELY
“ REPUBLIC OF TANZANIA ”
DURING THE NATIONAL COMPETITION DAY IN
19TH NOVEMBER 1964
WAKAL
MINISTER FOR INFORMATION AND
TOURISM
Barua hiyo pia ilisema...
Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita
ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na wewe
pamoja na wananchi wenzio 16 ulishauri nnchi
yetu iitwe Tanzania . Nafurahi kukuarifu kuwa
mshirikiane ile Zawadi ya sh. 200 iliyoahidiwa
na leo nakuletea check ya sh. 12/50 ikiwa ni
hisa yako katika zile sh.200. Nashukuru sana
kwa jitihada ya kufikiri jina la Jamuhuri yetu.
Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil Waziri
wa Habari na utalii kipindi hicho.
Sasa kwa nini Mohamedi Iqbal Dar anadai yeye
kuwa mshindi pekee wakati barua ilikuwa
inaonyesha kulikuwa na washindi wengine 15
ambao nao walishinda?
Jibu ni kuwa wakati wa kutolewa kwa Zawadi
hizo hakuna aliyejitokeza zaidi ya Bwana
Mohammed Iqbal Dar na Bwana Yusufal Pir
Mohamed ambaye hata hivyo alikosa sifa baada
ya kushindwa kutoa barua ya kumpongeza kuwa
ameshinda kwa madai kuwa Barua ameipoteza,
hivyo Wizara ya Habari na Utalii iliamua
kumtangaza bwana Mohammed Iqbal Dar kuwa
Mshindi na kumpatia zawadi yote ya sh.200/;
pamoja na Ngao.
Bwana Mohammedi Iqbal Dar anasema
anachosikitika ni kuwa mchango wake bado
Watanzania hawathamini mchango wake lakini
yeye anaipenda Tanzania na anajivunia kuwa
Mtanzania japo anadhani dini yake ya Uislamu
ndiyo tatizo hawataki kutambua mchango wake
ila anaamini kuwa siku moja ukweli utajulikana.
Hayo ni maelezo ya Mohammed Iqbal Dar
ambaye kwa sasa anaishi Uingereza kwa kuwa
huko ndiko alipata kazi eneo la Birmigham b35
6ps UK , Dar– es-Salaam House, 18
TURNHOUSE ROAD , PHONE 44 121-747-9822
Nimeona niwatumie hii wadau wangu ili tuweze
kuongeza ufahamu na kama ulikuwa unalijua
hili basi nimekukumbusha pia mambo
yalivyokuwa miaka ya 1964

0 comments:

Post a Comment