WAKUBWA TU!!.. JINSI YA KUSAFISHA UKE


Awali nilikuwa nikidhani kuwa kila mwanamke
anapaswa na anafahamu jinsi ya kujisafisha
ndani ya uke mara tu baada ya kuondolewa
bikira (kuanza mahusiano ya kimapenzi na
hatimae ngono), lakini nimekuja kugundua ukweli
kwamba wanawake wengi hawajui uke
unasafishwa vipi?
Baadhi huofia kuwashwa na sabuni na wengine
hudhani utokwaji wa utoko ni kawaida hivyo
hawana budi kuacha kama ilivyo na badala yake
hutumia “pads” ndogo au “wipes” zenye
manukato ili kuzuia harufu/shombo ya uke na
vilevile kuzuia uchafukwaji wa “vyupi” vyao.
Huitaji kuficha(Bali punguza) harufu ya asilia ya
uke kwa kutumia bidhaa zenye mahukato hasa
ukiwa na mpenzi wako kwani hiyo harufu ndio
uanamke wenyewe na ikikutana na ile ya kiume
ndio raha ya kufanya mapenzi na ikiwa mpenzi
wako ni“aliyejaaliwa” atakuwa akiipenda harufu
hiyo na hubaki akilini mwake hali inayoweza
kumfanya akupende zaidi au kutoweza kufanya
ngono na mtu mwingine bali wewe.
Hujawahi kusikia wanaume wanashindwa kutoka
(date) wanawake wengine baada ya wapenzi
wao kufariki dunia? Au mwanaume kushindwa
kuendelea na maisha yake ya kimapenzi bila
wewe na matokeo yake hata mkiachana lazima
atarudi tu kwako….sababu moja wapo ni hiyo.
Kujiswafi ili kupunguza ukali wa shombo/harufu
ya uanamke:
Utoko hujikusanya ikiwa mwili umetulia (usiku)
hivyo hakikisha unajisafisha kila asubuhi kabla
hujaanza kuoga.
Kwa wale tunaoishi Bongo wengi tunatumia maji
ambayo usalama wake ni wa utata, sasa ili
kuepuka maambukizo hakikisha maji ya
kujisafishia sehemu zako za siri yamechemshwa
vizuri. Unaweza kutenganisha maji ya kuoga na
ya kusafishia uke ukitaka.
*Kabla hujaguza uke wako hakikisha umesafisha
mikono yako vizuri kwa sabuni (ukiweza tumia
sabuni yenye dawa) na wakati huo huo pitisha
sabuni juu ya uke wako ili kuondoa vijidudu
kama vilikuwepo, safisha mahali hapo(juu ya uke
kwa maji na hakikisha hakuna sabuni).
*Kisha kwa kutumia kidole chako cha kati, ingiza
taratibu pale ambapo uume unaingia, kwa
kuanzia huitaji kwenda mbali sana. Zunguusa
kidole hicho taratibu huku ukijimwagia maji kwa
kutumia mkono wa pili, kisha kitoe (kitatoka na
weupe mzito) safisha kidole na maji yako.
*Rudia tena na sasa kiingize ndani zaidi na
ukizunguushe tena (huku ukijimwagia maji) na
kukitoa utaona “utoko” mwingi zaidi kidoleni,
rudia hatua hizo mpaka uhakikishe kidole
kinatoka bila weupe(utoko) na utahisi hali ya
usafi, hakuna utelezi.
Unapojimwagia maji ukeni huku kidole kiko ndani
maji huingia pia ukeni na ndio maana mwishoni
kabisa utahisi umesafishika vema kabisa na
utoko huo hautotoka tena siku nzima na uke
wako hautokuwa na shombo kali kama ambavyo
siku zote ambazo ulikuwa hujisafishi.
Kwa wale wanaotumia “bath” au “shower”
unafanya kama nilivyoeleza ila tofauti ni kuwa
maji yataingia vizuri zaidi ikiwa unapata “bath”
hivyo hakikisha “bath” sio ya kuchangia, maji ni
salama(safi), usiweke sabuni (bath cream) au
bidhaa yoyote yenye kemikali kwenye “bath”
yako ili kuepuka matatizo ya kiafya na
maambukizo mengine.
Ikiwa unaswali, nyongeza, ushauri, maoni kuhusu
mada hii na nyingine zilizopita tafadhali
niandikie.
Asante kwa uvumilivu na ushirikiano wako

0 comments:

Post a Comment