ROSE NDAUKA:NAFUNGA NDOA SIKU SI NYINGI

MSANII maarufu wa sinema za Kibongo, Rose
Ndauka amesema kuwa watu wasiwe na
wasiwasi kwani kwa mipango ya Mungu atafunga
ndoa na mzazi mwenzake Maliki Bandawe hivi
karibuni.
“Si muda mrefu mambo yatakuwa mazuri
tulikuwa tunaendelea kujuana, nadhani sasa
tunafahamiana vizuri hivyo watu wasiwe na
shaka, tutafunga ndoa soon,” alisema.
Rose ambaye hivi karibuni alihamasisha zoezi la
usafi na kuungwa mkono na wasanii mbalimbali
akiwamo Meya wa Ilala Jerry Slaa, alisema watu
wasihofu kuhusu ndoa hiyo kwani ipo njiani.
“Hatujui labda kuchelewa kwetu kuna kitu Mungu
amekiepusha, siku zote haraka haraka haina
Baraka,” alisisitiza Ndauka ambaye amepanga
kutembea Tanzania nzima kuwahamasisha
wananchi kuzingatia usafi.

0 comments:

Post a Comment