PROF JAY KUTUMIA MBINU ZA LADY JAYDEE NA MPOTO KUSAMBAZA ALBUM


Licha tatizo la usambazaji wa album bongo
lililowafanya wasanii wengi kusitisha kutoa
albums kwa kuhofia kupata hasara, rapper
Joseph haule aka Professor Jay ameahidi
kutoa album mpya mwaka huu (2014),
ambayo itakuwa ni album yake ya tano.
Rapper huyo mkongwe ambaye hivi karibuni
ametoa single mpya iitwayo ‘Kipi sijasikia’,
amesema ana mpango wa kutumia njia
walizotumia Lady Jaydee na Mrisho Mpoto
katika kusambaza album zao zilizopita,
kusambaza album yake mpya itakayoitwa
‘Izack mangesho’.
“Kweli sasa hivi kwa wadosi pale
kunasumbua…lakini tuna mpango wa
kuongea pia na Max Malipo”, amesema
Professor Jay kupitia Magic Fm. “Unajua
Max Malipo wapo karibu kila sehemu
kwahiyo wanaweza kusambaza kazi zetu.
Kama Mrisho Mpoto alianza kuuza album
yake kwa style hiyo..hata dada Jaydee pia
naona aliiuza mwenyewe kwa style hiyo..so
na mimi nadhani naweza kupitia njia hiyo
lakini kwa kuiboresha zaidi”.
Album za Professor Jay zilizopita ni
‘Machozi Jasho na Damu- 2001’,
‘Mapinduzi Halisi -2003’, ‘J.O.S.E.P.H-
2006’, na ‘Aluta Continua -2007’.

0 comments:

Post a Comment