PENZI LA WASTARA LAMNOGEA KALA JEREMIAH...!!! KALA AFUNGUKA NA KUWEKA KILA KITU WAZI KABISAAA..!!


MKALI wa muzi Bongo Kala Jerimiah "Kala"
amesema kwamba msanii nyota wa kike wa
Bongo movie Wastara Juma "Wastara" ndiye
mwenye sifa zote za mwanamke ambaye
anahitaji kuishi naye.
Kala aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita
alipoongea na mwandishi wa habari hizi na
kuongeza kwamba kila awazapo suala la kuwa
na mke basi mawazo yake huenda kwa Wastara
kwa kuminganisha na sifa zake.
"Siyo Siri, Wastara ndiye mwenye sifa za kuwa
mke wangu mtarajiwa. Si kwamba namtaka yeye
hapana ila nahitaji mwanamke mwenye sifa
kama zake. Namkubali sana Wastara. Napiga
picha jinsi alivyovumilia kwa mengi. Ndoa yake
na marehemu Sajuki ilikumbana na changamoto
nyingi sana. Mpaka sasa amekomaa bila
kuolewa na maisha yanasonga kama kawaida.
Dah! kwa kweli nikipata mke kama huyu
nitafurahi sana japo wapo wachache sana
Duniani" Alisema Kala Jeremiah.
Akieleza ni kwanini amefikia hatua ya
kuzungumzia suala la ndoa na kama anampango
wa kuoa, Kala alisema kwamba yeye ni
mwanaume mwenye sifa zote za kuoa na ni
lazima ataoa hivyo si ajabu kuzungumzia suala
hilo.

0 comments:

Post a Comment