MWANAUME ANASWA NA SEMBE NEW YORK CITY/USA AKITOKEA BONGO


Wiki iliyopita, mtu mmoja mwenye uraia wa
Ghana kwa jina Boubacar Traore (42),
alikamatwa na kilo 3.5 za heroin zenye
dhamani ya dola za Kimarekani milioni 3
mara tuu baada ya kuwasili katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa JFK, jijini New
York, Marekani. Aliwasili uwajani hapo kwa
ndege ya British Airways ikitokea London
alikounganisha ndege.
Taarifa zilizowasilishwa mahakamani
zinaonyesha kuwa Traone alianzia safari
yake Tanzania lakini haijaelezwa alipitia
JNIA au KIA. Hata hivyo, jana Rais Kikwete
alisema kuwa kuwa dawa za kulevya
zinazidi kupita katika viwanja vya ndege
vya JNIA na KIA na kuwa hali hii inazidi
kuchafua heshima na jina la Tanzania.
Maafisa uwanjani hapo (JFK) walishtukia
begi moja (Samsonite roller bag) ambalo
lilikuwa limekaa kama halina mwenyewe
vile. Baada ya kulichunguza walikuta kuwa
mmiliki wake alikuwa ni Traone ambaye ni
baba wa watoto saba anayemiliki grocery
nchini Ghana. Baada ya begi hilo
kupekuliwa maafisa hao walikuta kilo 3.5
za heroin zilizokuwa zimefichwa kwenye
begi hilo kama linavyoonekana kwenye
picha hapo chini.
Baada ya kukamatwa Traore alikiri kosa
lake la kushiriki katika kujaribu kuingiza
dawa hizo za kulevya Marekani na kukubali
kushirikiana na polisi ili kumkamata
mshiriki mwingine. Baada ya kupiga simu
kadhaa, Traore alikubaliana kwenye simu
kukutana na mtu mwingine kwa jina Francis
Abankwa (50) ambaye ni devera wa moja
ya mabasi ya MTA (Metropolitan
Transportation Authority).
Abankwa alikuwa amepanga kuchukua
mzigo mida ya saa kumi jioni lakini
alimwambia Traore asubiri kidogo mpaka
round ya mwisho kwa sababu basi lilikuwa
limejaa abiria wengi. Hivyo, walikubaliana
kukutana saa 6.51 za jioni kwa saa za New
York katika kituo cha basi cha Grand
Concourse and East Tremont kilichopo
Bronx, jijini New York. Wakati huo, Abankwa
alikuwa bado hajui kuwa Traore alikuwa
tayari ameshakamatwa na dawa hizo. Pia
hakujua kuwa alikuwa amekubali
kushirikiana na Homeland Security
kumkamata na yeye pia.
Baada ya Abankwa kuwasili katika kituo
cha basi cha Grand Concourse and East
Tremon na basi lake, Traone alipanda
kwenye basi hilo akiwa na begi lililokuwa
na dawa hizo za kulevya. Baada ya
kupanda basi, Abankwa aliendesha basi
lake huku wakijadiliana juu ya dili lao la
dawa za kulevya. Mazungumzo yao yote
yalikuwa yanarekodiwa na kifaa ambacho
Traore alivalishwa na polisi.
Pia kwenye basi hilo kulikuwa na maafisa
wawili waliokuwa wamevaa nguo za kiraia
na walipanda basi mapema kabisa kutokea
huko lilipoanzia na kujifanya kama abiria
wa kawaida. Maafisa hao walishuka kituo
cha pili kabla y kufikia kituo cha mwisho.
Baada ya basi kufika kituo cha mwisho,
abiria wote waliobakia walishuka ispokuwa
Traore aliyebakia kwenye basi na kurudi na
dereva Abankwa hadi kwenye depot ya
mabasi ya MTA (Kingsbridge Depot) iliyopo
Inwood.
Baada ya kuliacha basi pale, walielekelea
kwenye gari ya Abankwa na ndipo polisi
wapowazunguka na kumkamata Abankwa
ambaye wakati huo alikuwa na lile begi
mikononi mwake. Abankwa ambaye yupo
katika kituo cha mahabusu cha
Metropolitan kilichopo Brooklyn
amefikishwa mahakami na kushtakiwa.
Traore nae ameshtakiwa lakini kwa mujibu
wa rekodi za kimahakama amepewa
dhamana kwa bond ya dola 100,000.
Abankwa amefanya kazi MTA miaka nane
na mwaka 2012 alilipwa dola za Kimarekani
102,000 kama mshahara pamoja na
marupurupu mengine. Mwezi February
mwaka huu alishtakiwa kwa fraud baada ya
kuchukua Medicaid benefits kwa ajili ya
mke na mtoto wake.

0 comments:

Post a Comment