MTOTO WA KAJALA AFUNGUKA KHS BEEF LA MAMAKE NA WEMA SEPETU

Kutokana na ugomvi unaoendelea kati ya Wema
Sepetu na Kajala Masanja,mtoto wa Kajala
aitwaye Paulette amesema anaumizwa na
ugomvi huo na kwamba amekuwa akimtumia
ujumbe Wema kumweleza anavyompenda.
Paulette alikuwa akizungumza na ‘Movie Leo’ ya
kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.
“Vimekuwa vinaniuma sana ila hata kama
wakisema vitu vyote ataendelea kuwa mama
yangu,” alisema. “Mimi naona mama yangu hana
makosa yoyote wanavyomtukana,mimi nakuaga
najisikia sana vibaya. Namwambia (Wema)
mama yangu Hata kama amekoseA kitu chochote
amsamehe kwasababu mimi nampenda Wema
kama aunt yangu na ninampenda mama yangu
tena sipendi nikiona wanatukanana wala nini
napenda wawe marafiki,nataka nimwambie
Wema nampenda sana,” alisema. Paula.

0 comments:

Post a Comment