Ali kiba ni mmoja wa wanamuziki walio kimya
sana kwenye upande wa kuongelea mambo yake
binafsi, haswa kimahusiano, au hata kujitangaza
kumiliki kitu kingine chochote cha thamani kama
ilivyo desturi ya wasanii wengi hapa town baada
tu ya kupata umaarufu, ila siri hufichuka haswa
pale kwa warembo hawa wanapoamua kumwaga
mpunga ndipo hapo unapoanza kujua yaliyo chini
ya kapeti.Hawa ni warembo waliowahi kukiri
kuwa walishawahi kuwa na mahusiano na Celeb
huyu mkongwe sana kwenye anga za muziki huu
wa Bongo Fleva.
Jackline Wolper.
Mapenzi ya hawa wawili inasemekana yalianza
enzi hizo ambapo wawili hao walikuwa bado
hawana majina kabisa hapa town, kila mmoja
wao akiwa yupo kwenye hustle zakutoka kila
mmoja akiwa natetea fani yake, ila kwa bahati
nzuri AliKiba akaanza kupata umaarufu kuitia
muziki hata kabla ya Wolper kuanza ku-make
headlines kupitia filamu, akiwa kama muigizaji.
“Ni kitambo kidogo sana wote hatukuwa star
lakini mwenzangu alifanikiwa kuchomoka,lakini
Ali ndiye aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa
Mapenzi” alifunguka Wolper,
“Ali akawa star,alipokwenda nje nikasikia
wanawake wanamshobokea,sasa mimi sikutaka
karaha nikakaa pembeni,lakini jamaa ni mtu poa
sana na tukikutana tuanasalimiana freshi kabisa”
alimalizia akizungumzia sababu zilizomfanya
aachane na Kiba wakati huo.
Lulu Michael .
haikujulikana mapema kama inavyotokea kwa
watu maarufu wengi hapa town, ila mahusiano
yao yalianza huko kitabo sana, baina ya Lulu na
Ali Kiba, ila mwisho wa siku Lulu aliamua
kumwaga mpunga hadharani kufunguka juu ya
mahusiano yao.
“Duh! Umenikumbusha mbali sana. Nilishasahau
kabisa kama niliwahi kutoka naye. Pamoja na
kwamba ni kweli alikuwa mtu wangu, lakini kwa
sasa moyo wangu hautaki kusikia kingine zaidi
ya Bieber na namuonea wivu sana Selena Gomez
(mpenzi wa Bieber).”
ila hakutaka kuzungumzia sababu za kuachana
naye, nakusea ilikuwa tu sababu zake binafsi
kwa sababu mapenzi yana taba moja kuwa
ukiyag’ngania hasa pale ambapo hauenjoy
mwisho wake ni kuumizana tu, alimalizia lulu
kuelezea safari yake ya mapenzi, na hadi hivi
sasa anakiri kuwa bado yupo yupo sana.
HAWA NDIO MASTAA WALIOKIRI KULA URODA NA ALIKIBA..SOMA HAPA WAKIFUNGUKA
3:17 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment