BAADA YA TIGO PESA! M PESA SASA INAKUJA FACEBOOK PESA DADEKIIII!

Miaka michache ijayo M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel
Money zinaweza kuwa na mpinzani mwingine,
Facebook Pesa!!
Katika miaka ijayo Facebook haitakuwa sehemu
tu ya kuandika status, kupost picha ama kusoma
kinachoendelea mjini bali itakuwa sehemu
ambapo watumiaji wataweza kufanya malipo ya
kieletroniki na kutunza fedha pia. Mtandao huo
wa kijamii unadaiwa kuwa kwenye mchakato wa
kuingia kwenye utoaji wa huduma za kifedha
ambapo pamoja na mambo mengine, wafanyakazi
waliopo nchi za kigeni wanaweza kutuma fedha
kwa familia zao.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Financial
Times, Facebook imetuma maombi kwenye benki
kuu Ireland, ambapo kama ikipewa itawaruhusu
watu kutunza fedha kwenye mtandao huo wa
kijamii, kuhamisha kwa watumiaji wengine na
kulipia bidhaa ama bili.
Pia mtandao huo umezungumza na makampuni
mapya ya huduma hizo ya London, TransferWise,
Moni Technologies na Azimo ambayo yanatoa
huduma za utumaji fedha kwa njia ya apps za
smartphone.

0 comments:

Post a Comment