ASHA BARAKA MKURUGENZI WA TWANGA AFUNGA NDOA YA SIRI

WERAWERAAA ! Baada ya kuishi kwa muda
mrefu tangu alipotengana na mumewe
Khamis Bwela , Mkurugenzi wa Bendi ya The
African Stars ‘ Twanga Pepeta ’ , Asha Baraka
‘ Iron Lady’ usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita
alifunga ndoa na mfanyabiashara maarufu
Dar aitwaye Idd Baka Pandisha ,
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, tukio hilo la
aina yake lilijiri maeneo ya Magomeni -
Usalama, Dar , nyumbani kwa mkurugenzi
huyo ambapo watu wachache ndiyo
waliohudhuria huku mdogo wa bi harusi ,
mama yake Nasibu Abdul ‘ Diamond ’ Sanura
Kasim a. k .a Sandra akiwa ndiye msimamizi
wa shughuli nzima.
“Yaani ukaribu wote huo na Asha Baraka
hamjaalikwa ( Global)? Basi kwa taarifa yenu
amefunga ndoa ya siri ili kujiweka sawa
katika pilika zake za kugombea ubunge, ”
alisema mtonyaji wetu aliyekuwa ndani ya
nyumba .
Baada ya kupata ‘ niuzi ’ hizo motomoto ,
Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Asha Baraka
ili kutaka kujua furaha yake ikoje baada ya
kufunga ndoa ambapo bila kutegemea
paparazi alikumbana na sauti ya maombi ya
kwamba asitiriwe.
“Ni kweli nimefunga ndoa lakini naombeni
mnisitiri kwani mtaniharibia kila kitu ,
chondechonde jamani mimi ni mtu wenu pia
ni kama dada yenu , ” alisema Asha Baraka.
Kwa muda mrefu Asha Baraka amekuwa
mwenyewe bila mume baada ya kutengana
na Bwela ambaye alimuoa mwigizaji Tamrina
Poshi ‘ Amanda ’ waliyetengana hivi karibuni .

0 comments:

Post a Comment