ANUNUA KESI ILI ALE UGALI WA BURE JELA!

Kisanga ! Njemba aliyetajwa kwa jina moja la
Jumanne ( 28 ) , ametiwa mbaroni na polisi
kwa msala wa kumchoma kwa bisibisi
mama’ ke mzazi aitwaye Habiba Said au
Mama Nyamsati na kumsababishia majeraha
makubwa kichwani .
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri hivi karibuni ,
maeneo ya Temeke -Pire jijini Dar ambapo
Jumanne alidaiwa kutenda unyama huo kwa
kumshambulia mama’ ke kwa fimbo kisha
kuchukua bisibisi na kumchoma nayo
kichwani kwa madai kuwa anataka kurudi
jela akale ugali wa bure .
Ilidaiwa kuwa baada ya wadogo zake
Jumanne kumuona kaka yao akidhamiria
kumuumiza mama yao ndipo wakaingilia kati
ili kumzuia, lakini Jumanne aliwapiga wote
na kumjeruhi mdogo wake mwingine kwa
bisibisi hiyohiyo .
Wakati tukio hilo likiendelea , majirani na
ndugu walikwenda kutoa taarifa katika Kituo
Kidogo cha Polisi cha Wailes , Temeke
ambapo polisi walifika eneo hilo na
kumkamata Jumanne huku mama yake
akipatiwa PF - 3 kwa ajili ya matibabu katika
Hospitali ya Temeke . Baadaye mtuhumiwa
huyo alihamishiwa Kituo cha Polisi
Chang’ ombe.
Ilifahamika kwamba mama huyo alishonwa
nyuzi kadhaa kichwani baada ya kujeruhiwa
vibaya .
Akizungumza na wanahabari wetu, mama
huyo alisema kuwa siyo mara ya kwanza
kwa mwanaye kumshambulia kama hivyo
kwani aliwahi kumshambulia kwa kumpiga
vichwa bila kujali kama alikuwa na mtoto
mdogo mgongoni ambaye ni mdogo wake
Jumanne .
“Huko nyuma alishawahi kunivamia nikiwa na
huyu mdogo wake mgongoni akanipiga
vichwa hadi uso wote ukavimba ,” alisema
mama mzazi wa Jumanne na kuongeza :
“Nilisimama naye mahakamani na akafungwa
miezi 6 kisha akaachiwa .”
Mzazi huyo alisimulia kwamba chanzo cha
mwanaye kuwa katika hali hiyo inawezekana
ni mambo ya Kiswahili ( kulogwa ) kwa
sababu siyo kawaida kwa mtoto kumpiga
mama’ ke .
Baada ya soo hilo kufikishwa kituoni hapo,
shitaka hilo lilifunguliwa jalada ya CH/
RB/2975 /14 KUJERUHI ambapo polisi
wanaendelea na uchunguzi ili jamaa
afikishwe mahakamani.

0 comments:

Post a Comment