AISHA MADINDA NA TUHUMA ZA KUIBA SIMU

Mnenguaji maarufu Bongo aliyewahi kutopea
kwenye matumizi ya madawa ya kulevya
kabla ya hivi karibuni kuamua kuacha,
amegandwa na skendo ya kuiba siku lakini
mwenyewe alipoulizwa , alishangazwa na
madai hayo huku akidai kuwa hawezi kufikia
hatua hiyo .
Mnenguaji maarufu Bongo, Aisha Madinda.
Awali chanzo chetu kilitunyetishia kwamba,
mdada huyo alizama kwenye saluni moja
iliyopo Kijitonyama na kuweka fresh nywele
zake lakini alipotoka tu mmoja wa wateja
akalia kuibiwa simu yake .
Kwa kuwa yeye ndiye aliyetoka muda ule
watu wakajua ndiye aliyechukua, walipotoka
kumuangalia ili wamuulize alikuwa
ameshatokomea, ” alidai mto habari huyo
aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Aisha Madinda akiwa kazini .
Mwandishi wetu alipozungumza na Aisha
kuhusu ishu hiyo alisema : “Niibe simu, mh !
Kweli ninaishi mitaa hiyo na mara mojamoja
nikitoka kazini nimechelewa naendaga saluni
lakini sijawahi kusikia wala kuitwa na mtu
akidai nimeiba simu.
Hao wanaonisema hivyo watakuwa na
sababu zao nyingine tu za kutaka
kunichafulia jina langu. ”

0 comments:

Post a Comment