UWOYA KUOLEWA TEANA NA TAJIRI WA MADINI


Baada ya kudaiwa kutengana na aliyekuwa
mumewe yaani Ndikumana Katauti toka nchini
Rwanda,
Star mkubwa wa filamu Swahiliwood Irene
Uwoya anadaiwa kuwa katika mishe mishe za
kufunga ndoa na jamaa mmoja mfanyabiashara
wa Madini mwenye pesa zake ambaye anaishi
Sinza, Dar es salaam. Habari zaidi zinadadavua
kuwa jamaa huyo ameoza kwenye penzi la
Uwoya ambaye alifunga ndoa ya kifahari na
Ndikumana miaka michache nyuma na kuishia
kuwa katika gogoro la mara kwa mara. Jamaa
ndiye anataka kumuoa Uwoya haraka
iwezekanavyo huku mashosti wa Uwoya
wakimshangaa star huyo kama ataiweza ndoa
hiyo baada ya kushindwa kwa Ndiku.
"Inashangaza sana kwasababu hata Uwoya
mwenyewe anaridhia hicho kitu, sasa sisi
mashosti zake tunajiuliza alishindwa nini kwa
Ndiku mpaka leo hii atake kuingia kwenye ndoa
mpya?" Chanzo kililiambia gazeti la Visa
Chanzo hicho kilizidi kumwaga habari kwa
kusema "huyo kijana kadata na Uwoya kwa
kweli, hasikii la bibi yake wala la shangazi zake,
kaamua na yeye ndiye kiherehere kutaka kumuoa
Uwoya, na hizo pesa zake ndizo zinazomzuzua
hata Uwoya mwenyewe"
Mashosti hao wa Uwoya walimalizia kwa
kusema kuwa hata hivyo Uwoya atakuwa na
wakati mgumu kwani mpaka sasa wazazi wake
hawajui kuhusu issue hiyo ya ndoa mpya
kwasababu wao ni waaminifu kwa dini yao ya
kikiristu na pia bado wanamtambua Ndikumana
kama mkwe wao kwasababu ndoa za kikiristu
huwa hazivunjiki.
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe
24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako
halisi.
at Friday, April 18, 2014

0 comments:

Post a Comment