Ni siku chache tu zimepita toka Paul Okoye wa
kundi la P-Square afanye harusi ya kimila na
mke wake Anita Isama huko Nigeria, lakini baada
ya wote wawili (Peter & Paul) kukamilisha
majukumu ya ndoa zao, kuna habari ambazo
zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi
baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square
ambao inasemekana sasa hawaelewani vizuri.
Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa kwa
mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa kumekuwa na
kutoelewana baina ya kaka mkubwa wa
mapacha hao Jude Okoye na mke wa mdogo
wake Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, kitu
kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao
mwaka jana.
Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya
Peter na Lola mwaka jana, lakini alihudhuria ya
Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya
watu waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina
yao.
Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi
huo unaomhusu Lola umesababisha Peter na
Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle
Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na
dancers wao.
Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu
ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na
ugomvi wao.
“After over 10 years of hard work, it’s over. (I)
Am done.” ikiaminika kuwa alimaanisha
amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa
yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha
katika maneno hayo machache.
After over 10yrs of hard work, it's over. Am
done.
— IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014
Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka
yote na kuproduce hits zao paomoja na kudirect
idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri.
Lakini kuna baadhi ya watu nchini Nigeria
wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa ugomvi
‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo
vya habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya
album yao mpya.
UGOMVI WA PETER & PAUL WA P-SQUARE, MKE WA PETER NA KAKA YAO INASEMEKANA NDIO CHANZO
3:07 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment