Mchezaji Sylvain Azougoui alifariki uwanjani
baada ya kupiga teke ya kichwani
Mchezaji wa klabu ya Ac Bongoville,Sylvain
Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke ya
kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini
Gabon.
Kipa huyo alifariki alipokuwa akipelekwa
hospitalini baada ya tokeo hilo wakati wa mechi
yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka
Togo alikuwa amelisimamisha kombora lililopigwa
langoni mwake, lakini mshambulizi alipoteza
mwelekeo na kumkanyaga Azougoui kichwani.
Mechi hiyo ya siku ya Jumapili ilichezwa
Bongoville ambalo liko umbali wa kilomita 800
kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon.
"Ni vigumu sana kushuhudia hali hii ya
uchungu ,'' ilisema taarifa katika mtandao wa
klabu hiyo.
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment