MAKUBWAAA!

Makubwa! Kaka mkubwa kunako gemu la
filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘ Ray The
Greatest’ amefunguka kuwa hana mpango wa
kumuoa mwanadada Chuchu Hans kama
inavyodaiwa na baadhi ya watu .
Vincent Kigosi ‘ Ray na Chuchu Hans wakiwa
katika pozi .
Akijibu swali aliloulizwa na wanahabari wetu
hivi karibuni , kuhusiana na kudaiwa kuwa
baada ya mpenzi wake huyo kupewa talaka
ana mpango wa kufunga naye ndoa kama
ilivyokuwa inadaiwa ambapo alikataa
katakata suala la yeye kufunga ndoa na
Chuchu.
Diva wa filamu za Kibongo Chuchu Hans.
“Sina mpango wa kuoa ndugu yangu, hayo ni
maneno ya watu ambayo yapo tu mitaani ila
kwa sasa niko njiani naenda gym baadaye
nitakutafuta tuongee .” alisema Ray .
Staa mkubwa kunako gemu la filamu za
Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ .
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa muigizaji
huyo kufunguka kuhusiana na suala la ndoa
na swali linakuja , je , Chuchu anafahamu
kuwa anachezewa tu ? Jibu analo mwenyewe
moyoni mwake .

0 comments:

Post a Comment