KUMBE DIAMOND ANA MTOTO??

Nani aliyekuwa anafahamu kuwa Diamond
Platnumz ni baba? Well, hatujawahi kumsikia
popote akisema kuwa ana mtoto lakini staa huyo
wa ‘My Number One’ alikuwa mkarimu wa
kutosha kuweza kuelezea ‘furaha ya kuwa mzazi’
kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao
maarufu wa Nigeria uitwao Lobatan Africa baada
ya kwenda huko wiki kadhaa zilizopita
alikoshirikishwa pia na mastaa wa huko
wakiwemo Waje na Dr Sid.
Kwenye mahojiano hayo, mtandao huo ulimuuliza:
What have you learnt about fatherhood, now that
you’re a father (umejifunza nini kuhusu ubaba
kwakuwa sasa wewe ni baba)
Diamond alijibu: Fatherhood is a great
experience, very humbling. You learn a lot about
your children and the kids and the kinds of
things they love. For example, my baby loves this
cartoon that has a catchy song, I think Ben10.
Hahaha!! (Kuwa baba ni kitu kikubwa, kinavutia
sana. Unajifunza mengi kuhusu watoto wako na
vitu wanavyopenda. Kwa mfano ‘mwanangu’
anapenda katuni hii yenye wimbo unaogusa,
nadhani Ben 10!
Bonyeza hapa kusoma mahojiano hayo
Kumbe Diamond ana mtoto tena mkubwa
anayeweza kuangalia na kuelewa katuni? Swali ni
kwanini hajawahi kusikika akisema ana mtoto?
Hata hivyo September mwaka jana, moja ya
magazeti ya udaku ya kampuni ya Global
Publisher, yaliandika habari ya kuibuka kwa
msichana aitwaye Sasha Juma aliyedai kuwa
amezaa na Diamond.
Sasha akiwa na mtoto anayedai ni wa Diamond
Msichana huyo alidai kuwa likutana na Diamond
Mlimani City jijini Dar es Salaam na akampenda
kwakuwa anafanana na Wema Sepetu (kipindi
hicho walikuwa wameachana. Gazeti hili lilisema
wawili hao hawakuchukua muda na wakaanza
uhusiano uliowafanya wakutane kimwili na
kupelekea msichana huyo kushika ujauzito.
Lilidai asha alimpa taarifa staa huyo ambaye
alimuomba asitoe mimba kwakuwa atamsomesha
msichana huyo aliyefukuzwa shuleni na pia
kuahidi kumlea mtoto huyo.
“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi
mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha
masomo na kusema kuwa ataniendeleza na
atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona
tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata
kila kitu,” gazeti hilo lilimnukuu Sasha.
Lilisema lilipomtafuta Diamond kwa simu ambaye
kwa sasa yupo nchini Kenya, alijibu: Hahahaaa…
mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli
huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori
nyingine achana na hiyo.”
So kama Diamond ana mtoto, huenda aliamua
kumkubali mtoto huyu na pengine ndiye mtoto
huyu anayependa kuangalia katuni ya Ben 10!

0 comments:

Post a Comment