JE WAJUA MAREHEMU GURUMO ALIMWANDIKIA WIMBO DIAMOND KABLA HAJAFARIKI, SOMA ALICHOKISEMA DIAMOND HAPA


Star wa Bongo fleva Diamond Platnumz
amesema kuwa siku chache kabla mwanamuziki
mkongwe wa muziki wa dansi Maalim Muhidin
Gurumo hajaaga dunia alikuwa amemuandikia
wimbo kama shukrani kwa kumpa zawadi ya
gari mwaka jana.
Platnumz amesema meneja wake Babu Tale
alimpa taarifa hiyo njema ya kuandikiwa wimbo
na Gurumo lakini kwa bahati mbaya mzee
Gurumo alifariki kabla hajamkabidhi wimbo huo.
“Juzi kampigia simu Tale akamwambia kuna
nyimbo nimemtengenezea Diamond kwasababu
kwa alichonifanyia mimi nimeshukuru sana cha
kumlipa mimi sina lakini nimemuandikia nyimbo”
amesema Platnumz kupitia 255 ya XXL ya
Clouds Fm.
“so alikuwa anamwambia Tale kama
ameniandikia nyimbo, so angependa anipatie
nikamwambia sawa. Kama siku tatu hivi nyuma,
jana ndio nasikia taarifa hizi so najiona kama
nimechanganyikiwa hivi.”
Platnumz ameongeza kuwa mara ya mwisho
kuonana na Gurumo ilikuwa ni takribani wiki tatu
zilizopita baada ya mwimbaji huyo mkongwe
kumsurprise kwa kuhudhuria katika show
aliyokuwa anatumbuiza Diamond kwa lengo la
kutaka kumwona na kumshukuru kwa zawadi ya
gari aliyompatia.
“Mara ya mwisho kukutna naye nilikuwa nafanya
show Coco akaja maskini ya Mungu mpaka
kwenye show…kama wiki moja nyuma kama
sikosei au wiki mbili. Akaja akasema nimekuja
hapa kukuona, alipenyapenya hadi akaweza
kufika pale…nilivyomuona anakuja ilibidi pale
nikatishe show nikamsalimia kidogo halafu
nikaendelea na show, halafu baadae nikawa niko
nae backstage na nini nikazungumza nae.So
akasema nimekuja kukushukuru sana sana sana,
akasema ningependa uje nyumbani nikamwambia
sawa.”Amesema Diamond.
Mwili wa marehemu mzee Gurumo umepelekwa
kijijini kwake Masaki, wilaya ya Kisarawe mkoa
wa Pwani kwaajili ya mazishi yanayofanyika leo.

0 comments:

Post a Comment