IREN UWOYA AFUNGUKA!

Uwoya: Range Rover nimeipata
kwa njia nyingine sio sanaa, akiri
‘maisha ya Instagram’ kwa
waigizaji hayatokani na sanaa
By Sandu George on April 16, 2014 (1 min
ago)
Baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo movie
wamekiri kuwa maisha mazuri na ya kifahari
ambayo huwa wanatuonesha kwenye Instagram,
hayatokani na kipato wanachokipata kupitia
sanaa ya uigizaji kwasababu ni kidogo
kulinganisha na maisha hayo.
Irene Uwoya ni miongoni mwa waigizaji waliokiri
hilo kupitia kipindi cha ‘Take One’ cha Clouds Tv,
na kuongeza kuwa majina wanayoyajenga kupitia
sanaa ndio yanayowawezesha kupata fursa
zinazowasaidia kuwa na maisha mazuri na sio
kipato cha kuigiza.
Mwaka jana Uwoya aliwahi kushare picha za gari
lake alilokuwa amenunua aina ya Range Rover-
evoque nyeusi, lakini amekiri kuwa gari hilo
hakulipata kwa pesa ya movie.
“Sipendi kuwa muongo napenda kuwa mkweli,
kweli nafanya sanaa inaniingizia hela, lakini
mambo ya evoque nimeyapata kupitia njia
nyingine, ”alisema Uwoya. “ambayo pia sanaa
ilinisaidia nikaipitia hiyo njia…boss wangu Ruge
alisema fursa, unaitumia fursa, kwahiyo nilipata
fursa ya kuingia kwenye sanaa na mimi
nikaitumia hiyo fursa kupata vyanzo vingine vya
hela nikainunua ile gari”.
Kama hiyo haitoshi Uwoya ameongeza kuwa sio
Range Rover pake yake ambayo iko chini ya
himaya yake, “sio moja Zamaradi yako mengi
mengi mno, kwahiyo unatumia fursa”. Upo?
Hata hivyo pamoja na Zamaradi kumbana
mrembo huyo ataje hiyo ‘njia nyingine’ jibu
lilikuwa hili: “Zamaradi hiyo ni siri yangu nikianza
kukwambia si wataniiga, haiwezekani siwezi
kukwambia”.
Haya kazi kwenu wasanii wa muziki kutumia
fursa kupitia majina yenu kupata ‘njia nyingine’
ya kupata maisha mazuri, ila hakikisha iwe ni njia
safi na halali.

0 comments:

Post a Comment