DUUH MAINDA ADAIWA KUTONGOZA WAUME ZA WATU KANISANI

OOHHOO! Mwigizaji mkubwa wa sinema za
Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ anadaiwa kuangua
kilio ‘laivu’ kanisani kisa kubanwa na waandishi
wa Global Publishers juu ya madai ya kupora
waume za watu na ishu ya kutaka kuolewa na
mchungaji hivyo kuzua ‘kitimbwili’ kwenye
nyumba hiyo ya Mungu.
Mwigizaji mkubwa wa sinema za Kibongo, Ruth
Suka ‘Mainda’ akilia.
ENEO LA TUKIO
Timbwili hilo la aina yake lilijiri kwenye Kanisa la
Kiroho la Huduma ya Inuka Uangaze lililopo
maeneo ya Sinza-Lion jijini Dar hivi karibuni
baada ya waandishi wetu kutinga kanisani hapo
kwa lengo la kuzungumza na mchungaji wake
aliyetajwa kwa jina la Mwamposa.
Ruth Suka ‘Mainda’.
Ishu kubwa ilikuwa ni kujua undani wa skendo
iliyoenea mjini kuwa, Mainda anadaiwa kukwapua
baadhi ya waume wa waumini wa kanisa hilo na
kwamba yupo kwenye maandalizi kabambe ya
kufunga ndoa na mchungaji.
ANAJIPENDEKEZA KWA WAUME ZA WATU?
Ilisemekana kwamba madai hayo yalirushwa na
baadhi ya waumini ikidaiwa kuwa Mainda
amekuwa na tabia ya kujipendekeza kwa baadhi
ya waume za watu huku wengine wakidai anataka
kuolewa na mchungaji.
MCHUNGAJI AFUNGUKA
Waandishi wetu walipozinyaka habari hizo
ambazo zilizua gumzo kwa baadhi ya watu hasa
kwenye mitandao ya kijamii, walifunga safari hadi
kanisani hapo ili kuzungumza na mchungaji huyo
baada ya Mainda kukataa kupokea simu ya
mapaparazi ambapo alipopatikana mchungaji
huyo alifunguka anachokijua juu ya skendo hiyo.
BOFYA HAPA KUMSIKIA MCHUNGAJI“Mainda ni
binti kama mabinti wengine ninaowalea kiroho
hapa kanisani na amekuwa akijituma sana.
“Mainda ni tofauti na waumini wasanii wengine
labda ndiyo sababu ya watu
kumchafua. “Kuhusiana na ukaribu na waume za
watu ni uongo, hao wanaoeneza habari hizo wana
nia ya kumchafua kabisa kwa sababu wameona
ametoka eneo lile na kumfuata Mungu,” alisema
baba mchungaji huyo. Mchungaji huyo aliendelea
kufunguka kwamba, Mainda amekuwa akikutana
naye na viongozi wengine siku ya Jumatatu
kwenye kamati yao ya utendaji kazi, si kwa
mengine na amekuwa mstari wa mbele kwenye
kazi za kujitolea huduma za
kanisani.
ANAJITUMA SANA KANISANI
“Unaweza kuamini kutokana na ufanisi wake wa
kazi na kujituma, ndiye muumini ambaye
tumempa nafasi ya kuwa mbele watu wanapotoa
ushuhuda kwa sababu ana uwezo kwa sasa na
amekuwa akifanya kila analoweza kuweka safi
mazingira ya kanisa,” alisema mchunga kondoo
huyo wa Mungu.
KUHUSU KUMUOA
Kuhusu suala la kumuoa Mainda, mchungaji
alisema kwamba yeye hana wazo la kumuoa
Mainda na wala staa huyo hajawahi kuingia
kwenye gari lake.
“Ni binti mwenye heshima sana na kila kukicha
anakuwa muumini mwenye uwezo wa kutoa
huduma kwa waumini wenzake,” aligongea
msumari.
MAINDA AOMBWA AFUNGUE MOYO
Baada ya mazungumzo hayo mchungaji
alimuomba msaidizi wake kumwita Mainda ili
aufungue moyo wake kwa kuzungumza na
waandishi wa habari ambao walikwenda pale kwa
lengo la kupata ufafanuzi.
KILIO CHA KUFA MTU
Hata hivyo, Mainda alipotoka tu na kuwaona
waandishi wetu alikataa kuzungumza na kuanza
kuangua kilio cha kufa mtu.
Kufuatia tukio hilo, waumini waliokuwa
wakiendelea na shughuli zao kanisani hapo
walimshangaa Mainda huku wakimbeba
msobemsobe kumpeleka pembeni na
kumbembeleza. “Maweee…Sitakiii…Nasema
sitakii…nyiii…waandishi wameniharibia sifa yangu,
sitaki kuongea nao jambo lolote,” alisikika Mainda
wakati akiangua kilio.
Kwa muda mrefu sasa, Mainda amekuwa
akitumia muda wake mwingi kanisani akisali na
kufanya usafi hivyo kuwa mfano wa kuigwa katika

0 comments:

Post a Comment