Vdeo bora ya mwaka number one

Rayc nae alikuwepo

Enrico mtayarishaj bora wa taarab

Fa akiongea kwa niaba ya fid q

Tuzo ingine mtunz bora

Jchameleon

Lulu nae alikuwepo

Ze stage...amazing

Vic kiman

Vanesa

Weusi:kikundi bora cha mwaka

Vanesa mdee me n u

Mwana FA akiwa media social lounge

Isha mashauzi muimbaji bora wa kike

KAJALA : SIMLIPI WEMA MIL .13 NG' O !


JAMBO limezua jambo ! Zile shilingi milioni 13
alizolipa staa mkubwa wa kike Bongo, Wema
Isaac Sepetu ‘ Beautiful Onyinye’ mahakamani
ili kumnusuru Kajala Masanja kwenda
gerezani, zinaendelea kusababisha fukuto na
sasa Kajala amejibu mapigo , akisema
hatamlipa Wema fedha hizo .
Malkia wa filamu za Kibongo , Kajala
Masanja .
Wema na Kajala wapo kwenye gogoro zito
kwa muda mrefu huku mashabiki wa mastaa
hao waliojipa majina ya Team Wema
( wanaomuunga mkono Wema ) na Team
Kajala ( walio upande wa Kajala ) wakiukuza
ugomvi huo kwa kushambuliana kwa maneno
makali kwenye mitandao mbalimbali ya
kijamii .
WEMA KUFUNGUKA
Katika gazeti hili , toleo namba 877 la Aprili
25- Mei Mosi, 2014 la wiki iliyopita, liliandika
habari ya Wema iliyokuwa na kichwa; Kwa
mara ya kwanza Wema afunguka , asema:
NAJUTA KUMLIPIA KAJALA MIL . 13!
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Wema
kufunguka baada ya bifu la kimyakimya la
muda mrefu ambapo alifafanua chanzo cha
bifu lao na namna anavyojuta kumlipia Kajala
fedha hizo .
“Kusema kweli najuta kumlipia ( Kajala ) ile
faini ya Sh . milioni 13. Bora angeenda jela
miaka saba kuliko kunisababishia matatizo
na maumivu kiasi hiki . Mimi sijawahi
kumsema vibaya K kisa eti nilimlipia fedha
hizo , ” alisema Wema katika gazeti hilo.
Alipoambiwa kama Kajala yupo tayari
kurudisha fedha hizo alisema :
“Kama anataka kunilipa , anilipe kisha aende
jela maana mimi sikumkopesha , nilitoa kwa
moyo. ”
Diva wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu
a.k .a ‘Beautiful Onyinye’.
HABARI ZA MOTO
Baada ya gazeti hilo kuruka mitaani na Kajala
kulipata ndipo akaeleza mambo mazito .
Akizungumza na mwanahabari wetu, Kajala
alisema katika vitu ambavyo Wema
anatakiwa kuvisahau ni pamoja na kumlipia
mahakamani hizo milioni 13.
“Siwezi kumlipa ng ’ o. Namlipa nini sasa na
kivipi? Kwani tulikopeshana ? Hakuna
anachonidai Wema , hata kama akisema
nimlipe, siwezi kufanya hivyo , ” alisema
Kajala .
Huku akimwaga machozi, Kajala aliendelea:
“Unajua haya mambo yanachukuliwa kirahisi
tu na wadandiaji wa mambo, ni vile watu
hawajui ni kwa kiwango gani hili suala
linaniumiza.
“Wema alinisaidia , alinilipia fedha
mahakamani wakati ambao nilikuwa na
uhitaji na sikuwa na zile fedha . Kama
asingejitokeza kunilipia nilikuwa nakwenda
jela .
“Lile ni jambo kubwa . Thamani yake
haifananishiki na fedha . Ule ulikuwa ni utu tu ,
sasa leo iweje ligeuzwe kuwa kama deni ?
Siwezi kufanya hivyo . ”
YUPO TAYARI KWA SULUHU
Kwa mara nyingine tena , Kajala alisema
kuhusu kupatana na Wema yupo tayari muda
wowote , maana haoni sababu ya kuendelea
kwa ugomvi huo.
Hii ni mara ya tatu Kajala kuzungumzia
suluhu akisisitiza : “Nakosa amani kabisa na
huu mzigo. Natamani kuutua . Nipo tayari
kukutanishwa naye hata leo tuyamalize. ”
HABARI YA MJINI
Habari ambazo zimeenea mjini lakini bado
hazijathibitishwa zinadai kuwa , Kajala
anajiamini kwa sababu anajua fedha
alizolipiwa na Wema si zake , zililipwa na
aliyekuwa mwanaume ( boyfriend ) wa Wema ,
yule kigogo wa Ikulu anayetajwa kwa jina la
CK.
“Lile lilikuwa agizo, Wema hakuwa na fedha
zote zile kwa ajili ya kumlipia Kajala . Alipewa
na CK na kuambiwa amlipie ili asiende jela , ”
alisema mmoja wa watu wa karibu na
mastaa hao kwa sharti la kutotajwa gazetini.
ETI ULIKUWA MPANGO !
Chanzo kinaendelea : “Alivyoingia mitaani, CK
akajiweka karibu na Kajala na kumweleza
mchongo mzima , kuwa yeye ndiye aliyetoa
hizo fedha kwa hiyo asiwe na wasiwasi .
“Ndiyo maana hata Wema na CK
walivyoachana ikawa rahisi kwa CK
kujimilikisha Kajala moja kwa moja kwa
sababu anaujua ukweli.”
Haya ni madai ya chanzo chetu ambayo
hayajathibitishwa na wahusika .
SAFARI ZA CHINA VIPI ?
Habari nyingine ambazo bado zinafuatiliwa ili
zithibitishwe, zinasema kuwa , safari nyingi za
Kajala kwenda China kwa mapumziko huwa
anamfuata au kuongozana na CK.
“Hata sasa hivi ( juzi Jumatano ) wapo
safarini China wanakula bata. Yaani haya
mambo yamejifunga sana . Yanahitaji hekima
sana kuyamaliza ,” aliendelea kudai.
BIFU HADI LINI ?
Wadau wa tasnia ya filamu Bongo, kwa
nyakati tofauti wamekuwa wakipiga simu na
kutuma ujumbe mfupi katika chumba cha
habari cha magazeti pendwa Tanzania ,
Global Publishers na kueleza jinsi ambavyo
mtaani kunazidi kuchafuka kuhusu sakata
hilo huku wengi wakiwataka wayamalize .
“Haya mambo yanakuzwa na watu . Hawa ni
wasanii wazuri, wana majina makubwa na
wanaendana, nashauri wazungumze ,
wayamalize. Bifu lao halijengi badala yake
linabomoa , ” Maimuna Sadallah wa Majani
Mapana, Tanga alieleza katika ujumbe wake.
Msomaji mwingine aliyejitambulisha kwa jina
la mama Mwaija mkazi wa Mbagala - Maji
Matitu , Dar alikuwa na haya ya kusema :
“Haya mambo ya wanangu Wema na Kajala
yananichoma sana. Napenda sana filamu
zao, nafurahia namna wanavyoshirikiana na
kusaidiana. Hebu wamlaani shetani .”
WAZAZI WAOMBWA KUINGILIA KATI
James Sukae wa Kimara -Baruti , Dar alisema :
“Hili jambo na umri wao naona ni kubwa
sana kwao kulimaliza . Tukisema tusubiri
wayamalize wenyewe, haitawezekana ila
litazidi kuwa kubwa .
“Kajala ana wazazi wake, Wema naye
kadhalika .
Tena hapa nisisitize, wazazi wanaopaswa
zaidi kushughulikia hili ni mama zao. Mama
Kajala na mama Wema wanatakiwa kukutana
na watoto wao ili wawakalishe na
kuzungumza.
“Kwangu mimi , mbele ya wazazi ni jambo
dogo sana. Hekima zao ni kubwa na bila
shaka watalimaliza kuliko kuacha likielea
kama ilivyo sasa . Wakipuuzia hili suala
litasababisha janga kubwa . ”
DAWATI LA IJUMAA
Bado tunaendelea kusisitiza kuwa , Wema na
Kajala ni mabinti ambao wanapaswa
kushikamana. Alichokifanya Wema kwa
kumtolea Kajala milioni 13 ulikuwa ni wema ,
kugombana kwa sababu nyepesi si jambo
zuri. Bado wanayo nafasi ya kuzungumza na
kuendeleza urafiki wao . – MHARIRI.